Mshambuliaji
wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa anakipiga Barcelona, Luis Suarez
ameikumbuka timu yake ya zamani ya Liverpool baada ya kufuzu kucheza
fainali ya Kombe la Vilabu barani Ulaya.
Suarez
aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuwapongeza baada
ya kuwafunga Villarreal 3-0 na hivyo kufuzu kucheza fainali ya UEFA
Europe League.
Suarez aliandika “Hongera Liverpool kwa kuingia fainali, Hongereni marafiki!!”
No comments:
Post a Comment