Meneja huyo ambaye alikuwa kwa presha kubwa tangu wiki kadhaa na akiambulia ushindi wa Mechi moja kati ya 10 na Klabu hiyo ikisimama nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu England Premier League wameamua kumtimua ili waweze kufanya mabadiliko yatakayo wajenga upya na kufanya vyema msimu mpya wa 2016/2016.
Klabu ya Everton imempiga kalamu mkufunzi wake Roberto Martinez baada ya kuifunza klabu hiyo kwa miaka mitatu.
Kilabu hiyo ya Martinez ilio katika nafasi ya 12 katika jedwali li ligi ya Uingereza ilishindwa 3-1 na mabingwa wa ligi Leicester siku ya Jumamosi na kupoteza 3-0 dhidi ya Sunderland siku ya Jumatano.
Everton ilipoteza katika nusu fainali ya kombe la FA na lile la Carling msimu huu.
Timu hiyo imeshinda mechi tano pekee nyumbani msimu wote na inatarajiwa kumaliza msimu huu ikiwa na pointi za chini zaidi tangu uzinduzi wa pointi tatu kwa ushindi wowote mnamo mwaka 1981.Klabu hiyo inatarajiwa kuthibitisha rasmi hatua yao. Kumekuwa na ongezeko la maandamano dhidi ya kocha huyo raia wa Uhispania kutoka kwa Mashabiki katika mechi zilizochezwa nyumbani.
No comments:
Post a Comment