Kwenye Mechi hii, Barca walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 36 kufuatia Javier Mascherano kupewa Kadi Nyekundu kwa kumvuta Jezi Kevin Gameiro aliekuwa akichanja mbuga kwenda kufunga.
Nao Sevilla walimpoteza Ever Banega kwa Kadi Nyekundu mwishoni mwa Dakika 90 na pia Daniel Carrico alietolewa mwishoni mwa Dakika za Nyongeza 30.
Ndani ya Dakika 90 zilizoisha 0-0, Sevilla, ambao Jumatano iliyopita huko Basel, Uswisi waliibwaga Liverpool 3-1 na kutwaa UEFA EUROPA LIGI kwa mara ya 3 mfululizo, wangeweza kufunga katika Dakika ya 50 kama si uhodari wa Beki wa Barca Gerard Pique alieokoa Shuti la mbali la Ever Banega ambalo likagonga Posti.
Hadi Dakika 90 Bao zilikuwa 0-0 na kila Timu kubaki Mtu 10.
Katika Dakika za Nyongeza 30, Barca walipachika Bao zao za ushindi kwenye Dakika za 97 na 122 kupitia Jordi Alba na Neymar.
Hii ilikuwa ni Fainali ya 37 ya Copa del Rey kwa Barca, wakipitwa tu na Real Madrid waliocheza 39, na kati ya hizo 37 Barca wameshinda 28.Na hii ni mara yap Ili mfululizo kwa Barca kuzoa Ubingwa wa La Liga pamoja na Copa del Rey kwani Mwaka Jana, Barca walitwaa Kombe hili kwa kuifunga Athletic Bilbao 3-1.
Timu hizi zitakutana tena mwanzoni mwa Msimu ujao kugombea Supercopa de España kwa vile Barcelona ndio Mabingwa wa La Liga kwa Msimu wa 2015/16.
Kawaida Kombe hilo hugombewa na Bingwa wa La Liga na aliebeba Copa del Rey.
No comments:
Post a Comment