SIMBA YATULIA KILELENI BAADA YA KUIFUNGA MBEYA CITY 2-0
Simba ilikuwa haijawahi kuifunga City kwenye Uwanja wa taifa tangu timu hiyo ilivyopanda kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mechi ya kwanza Simba ilitoka sare ya kufungana kwa bao 2-2 dhidi ya Mbeya City kisha ikakubali kichapo cha goli 2-1 kwenye mchezo wa pili kabla ya leo kuikandamiza kwa mabao 2-0.
Simba inafanikiwa kurejea kileleni mwa VPL kwa mara pili msimu huu
Simba inapanda kileleni mwa ligi kwa mara ya pili msimu huu baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza ilipoifunga Stand United kwa bao 2-1 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na kufanikiwa kukaa kileleni kwa mara ya kwanza Febuary 13, 2016 tangu ifanye hivyo misimu mitatu iliyopita.
Ubingwa wa VPL bado mweupe kwa timu tatu za juu
Simba, Yanga na Azam zote zinaweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu kutokana na idadi ya pointi ambazo zinazitofautisha timu hizo pamoja na tofauti ya michezo huku idadi ya mechi zilizosalia ili ligi kumalizika ikipewa uzito wa wa juu kuamua nani atatwaa ubingwa msimu huu.
Simba imevunja mwiko wa kuteswa na Mbeya City kwenye uwanja wa taifa
Timu hizo tayari zimekutana mara tatu kwenye uwanja wa taifa huku Simba ikishindwa kutamalaki mara mbili mbele ya City, lakini leo imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza wa bao 2-0 na kuzima historia iliyokuwa imewekwa na wana-Mbeya hao.
Ushindi dhidi ya Mbeya City unamaana gani kwa Simba?
Baada ya kupoteza mechi yao dhidi ya Yanga, Simba inafanikiwa kushinda mbele ya Mbeya City na kupata matumaini makubwa ya kuwania ubingwa msimu huu tofauti na endapo wangepoteza mchezo au kutoka sare.
Nini kinafuata kwa timu hizo baada ya mchezo wa leo?
Simba itakuwa kwenyeji kwenye uwanja wa taifa ikiikaribisha Ndanda FC ya Mtwara March 10 mwaka huu wakati wakali wa Halmashauri ya jiji la Mbeya, Mbeya City wenyewe pia wataialika Coastal Union kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Post a Comment