MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema Kiungo wao Alex
Oxlade-Chamberlain atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 6 hadi 8 lakini
hahitaji upasuaji baada ya kuumia Goti walipofungwa 2-0 na Barcelona
Februari 23 kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Oxlade-Chamberlain, mwenye Miaka 22, alilazimika kuondoka Uwanjani Emirates mara baada ya kufungwa na Barca huku akitumia msaada wa Magongo kutembelea.
Arsenal, ambao walichapwa 3-2 na Man United Jumapili iliyopita huko Old Trafford kwenye Ligi Kuu England, Jumatano Usiku wako kwao Emirates kucheza na Swansea City Mechi ya Ligi.Arsenal wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi wakiwa Pointi 3 nyuma ya Tottenham na Pointi 5 nyuma ya Vinara Leicester City.
Wakitoka kwa Swansea City, Arsenal wana kibarua kigumu huko White Hart Lane kwenye Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao wa Jadi, Tottenham hapo Jumamosi Machi 5.

No comments:
Post a Comment