Conte amehusishwa na nafasi ya umeneja iliyo wazi Chelsea na tangazo lake litaongeza uwezekano kwamba huenda akahamia Stamford Bridge.
Mkufunzi huyo wa umri wa miaka 46 aliteuliwa meneja wa timu ya taifa ya Italia Agosti 2014 muda mfupi baada ya kujizuulu wadhifa wake kama kocha wa Juventus.
"Anahisi kwamba anahitaji kuwa uwanjani zaidi, kuongoza mazoezi kila siku,” Rais wa Shirikisho la Soka la Italia Carlo Tavecchio amesema.
Chelsea walimfuta kazi meneja wao Jose Mourinho Desemba 2015 na wakamteua Guus Hiddink kuwa kaimu meneja hadi mwisho wa msimu.
No comments:
Post a Comment