Wiki mbili zilizopita Timu hizo mbili zilitoka Sare 1-1 huko Moscow na hii ni Mechi ya 4 katika Kundi B ambalo hadi sasa Timu zozote 2 kati ya hizo 4 zinaweza kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya Timu 16. Man United wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na ubutu wa Magoli kwani hawajafunga Bao lolote katika Dakika 90 tangu Anthony Martial aliposawazisha walipotoka 1-1 na CSKA Moscow nah ii ni Jumla ya Dakika 325 za Michezo.
Tangu hapo, Man United imeambua Sare za 0-0 mara 3, mbili zikiwa za Ligi Kuu England dhidi ya Man City na Crystal Palace na moja na Middlesbrough katika Capital One Cup ambalo walitolewa kwa Penati 3-1.
Wakati Man United wapo Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England, CSKA wao Jumamosi waliendeleza uongozi wao wa Ligi Kuu ya Russia na kuwa Pointi 9 mbele baada ya kuichapa FC Ufa 2-0.
CSKA hawajafungwa katika Mechi 10 zilizopita na wanaongoza Ligi yao kwa kushinda Mechi 11 katika Mechi 14.
Hali za Wachezaji
Baada ya kuikosa Mechi na Palace, Phil Jones amepona na anaweza kucheza Mechi hii ya Leo lakini ipo hatihati kwa Antonio Valencia, Memphis Depay na James Wilson ambao wana maumivu na pia wapo Majeruhi Paddy McNair na Luke Shaw.
Kwa CSKA, ambao wako chini ya Kocha Leonid Slutski, Vasili Berezutski ni Majeruhi na ipo hatihati kwa Roman Eremenko ambae ana tatizo la Nyonga.
Man United wanaingia Old Trafford wakisaka ushindi wa kwanza dhidi ya Klabu ya Russia Uwanjani hapo baada huko nyuma kutoka Sare 3.
Man United walitoka 0-0 na Torpedo Moscow Msimu wa 1992/93 na pia Rotor Volgograd kutoka Sare 2-2 kwenye Raundi ya Kwanza ya UEFA CUP.
Msimu wa 2009, Man United walitoka Sare 3-3 na CSKA Moscow.
Mechi nyingine ya Kundi B hii Leo ni huko Uholanzi wakati PSV Eindhoven ikicheza na VfL Wolfsburg
No comments:
Post a Comment