Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Malale Hamsini Keya amewatangaza wachezaji 29 watakaounda timu ya taifa ya Zanzibar maarufu kama Zanzibar Heroes kwa ajili ya kushiriki mashindano CECAFA Challenge Cup yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Akitaja majina ya wanandinga hao, kocha huyo amesema wachezaji walioitwa wamekidhi vigezo vyote ikiwemo uzoefu wa kimataifa.
Wachezaji hao 29 waliochaguliwa leo hii kama wafuatao:-
WALINDA MLANGO
Mwadini Ali (Azam), Mohamedi Abrahman ‘Wawesha’ (JKU), Mohamed Ali ‘MUALI’ (Tanzania Prisons) na Idrissa Ali (Hard Rock).
WALINZI WA PEMBENI
Mwinyi Haji ‘Bagawai’ (Yanga), Nassor Massoud ‘Cholo’ (Stand United), Samir Haji Nuhu (Simba), Adeyum Saleh (Coast Union) na Consona Malik (JKU).
WALINZI WA KATI
Nadir Haroub ‘Canavaro’ (Yanga), Agrey Morris (Azam), Khamis Ali ‘Chichi’ (KMKM), Said Mussa ‘Kidindi’(Mafunzo) na Issa Haidari ‘Mwalala’ (JKU).
VIUNGO
Awadhi Juma (Simba), Mudathir Yahya (Azam), Said Makapu (Yanga), Mohammed Abdulrahman ‘Mbambi’ (Mafunzo), Khamis Mcha ‘Viali’ (Azam) , Ismail Khamis (Azam), Rashid Abdallah (Mafunzo), Suleiman Kassim Selembe (Stand united), Omar Juma (Hard Rock) na Mbarouk Chande (JKU).
WASHAMBULIAJI
Ibrahim Hilika (Zimamoto), Jaku Joma (Mafunzo) Matteo Anton Simon (Yanga) Abrahman Othman ‘Chinga’ (Jangombe Boys) na Ame “Ali ‘Zungu’ (Azam).
Kikosi hicho kinatarajia kufanya mazoezi yake Jumatatu November 9 kwenye uwanja wa Amaan saa 12:30 asubuhi ambapo mjumbe wa kamati ya muda ya ZFA Massoud Attai amesema hana taarifa ya kuzuiliwa kwa uwanja wa Amaan kwani hajapewa barua mpaka leo na siku ya Jumatatu wataanza mazoezi kwenye uwanja huo.
No comments:
Post a Comment