MABINGWA
wa soka Tanzania Bara Yanga leo wameondoa unyonge wa kufungwa na Simba baada
ya kuibuka kidedea kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezaji
wazamani wa Simba, Amisi Tambwe aliinyoosha timu yake hiyo ya zamani baada ya
kufunga bao dakika moja kabla ya mapumziko
kwa shuti kali la guu la kushoto akiwa ndani ya boksi akipokea pasi
kutoka kwa Malimi Busungu.
Busungu
aliyeingia uwanjani akitokea benchi, alirekebisha makosa yake alipoipatia Yanga
bao la pili katika dakika ya 79 alilofunga kwa kichwa akiunganisha mpira
uliotupwa na Mbuyi Twitte.
Busungu
kabla ya kufunga bao hilo, alipoteza nafasi ya wazi katika dakika ya 72 baada
ya kushindwa kufunga licha ya kuwa katika nafasi nzuri.
Simba
ambayo ilitawala zaidi kipindi cha kwanza, ilikuwa ya kwanza kulilifikia lango
la watani zao Yanga lakini krosi ya Hassan Ramadhani ilidakwa na Ally Mustapha.
Katika
dakika ya sita, Simba walilifikia tena lango la Yanga na kusababisha mpira kuwa
kona, lakini haikuzaa matunda baada ya kudakwa na Mustapha, ambaye aliumia
kabla ya kupatiwa matibabu na kuendelea na mchezo.
Simba
ilifanya shambulio la nguvu katika dakika ya tisa, lakini Mwinyi Kazimoto akiwa
amebaki yeye na kipa wa Yanga Mustapha, alipiga mpira ukagonga nyavu za nje.
Beki
wa Simba Juuko Murahid alioneshwa kadi ya njano kwa kumshika mshambuliaji wa
Yanga Donaldo Ngoma.
Hamisi
Kiiza nusura aipatie Simba bao la kuongoza katika dakika ya 13 baada ya beki wa
Yanga, Nadir Haroub kuchanganyana na kipa wake Mustapha, lakini alishindwa
kuuweka kimiani.
Kiiza
tena nusura afunge katika dakika ya 27 baada ya kupiga shuti kali ambalo
liliokolewa na kipa wa Yanga Mustapha.
Katika
kipindi cha kwanza Yanga walishindwa kung’ara katika safu ya kiungo ambayo ilishindwa
kuunganisha mabeki na washambuliaji na hadi kumfanya kocha wao kumtoa Simon
Msuva.
Dakika
ya 37 Kiiza alishindwa tena kuujaza mpira wavuni kufuatia krosi ya Said Ndemla,
baada ya mpira wa kichwa kupaa juu ya lango.
Awadhi
Juma alishindwa kufunga licha ya kuwa katika nafasi nzuri ya kufunga, lakini
alipiga mpira nje.
Yanga
walipata pigo baada ya mchezaji wake Mbuyi Twitte kutolewa nje kwa kadi
nyekundu na mwamuzi Israel Nkongo baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano.
Huu
ni mchezo wan ne Yanga inashinda na hivyo kuzidi kukalia kiti cha uongozi
katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kujikusanyia pointi 12 huku Simba ikipokea
kichapo cha kwanza na kubaki na pointi zake tisa.
Mbali
na ushindi huo, Yanga ambayo imecheza nyumbani mechi zote kabla ya jana,
ilishinda 2-0 dhidi ya Coastal Union, 3-0 dhidi ya Prisons na 4-1 dhidi ya JKT
Ruvu.
Wenzao
Simba kabla ya kibano cha jana walishinda ilishinda mechi mbili Tanga 1-0 dhidi
ya African Sports na 2-0 dhidi ya Mgambo JKT, kabla ya kuifunga Kagera Sugar 3-1
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga
wiiendi ijayo itacheza mchezo wake wa kwanza ugenini wakati itakapoifuata
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Simba wataendelea
kucheza Uwanja wa Taifa wakati watakapokaribisha Stand United ya Shinyanga.
Vikosi; Simba: Peter Manyika, Hassan Ramadhani/Paper Abdoulaye,
Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Said Ndemla,
Mwinyi Kazimoto, Mussa Mgosi/Ibrahim Ajibu, Hamisi Kiiza na Awadhi Juma.
Yanga: Ally Mustapha, Mbuyu Twitte, Haji Mwinyi, Nadir
Haroub, Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Simon Msuva/Malimi Busungu, Salum
Telela/Said Makapu, Amiss Tambwe/Deus Kaseke, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.
Mechi
zingine jana: Stand United iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT,
Tanzania Prisons ilishinda 1-0 dhidi ya Mgambo JKT, Coasta Union ilitoka suluhu
na Mwadui ya Shinyanga na Mtibwa Sugar iliilaza Majimaji kwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment