Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 17, 2015

SIMBA IMEVUNJA ‘MWIKO’ TANGA, ITAWEZA KWA KAGERA SUGAR?

Simba-Day

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Kwanza kabisa niwapongeze Simba SC, kitendo cha kukusanya alama sita katika uwaja wa Mkwakwani, Tanga ndani ya siku nne ni kipya kabisa kwao, lakini mwisho wa siku Simba imefanikiwa kushinda 1-0 dhidi ya African Sports na 2-0 dhidi ya JKT Mgambo. Ni mwanzo mzuri, tena ushindi mzuri wameupata katika moja ya viwanja vigumu kwa timu za Dar es Salaam.
Awali sikuwa na imani, niwe mkweli licha ya kutambua vipaji vipya katika timu na uwepo wa benchi la ufundi jipya tena lililopangiliwa ila bado sikuwa na imani na safu ya utawala ambayo ‘ilikuwa na mazoea ya kupaniki’ na hivyo kupunguza uwajibikaji wa timu.
DYLAN KERR
Mwalimu huyo raia wa Uingereza pengine ni mapema mno kuweza kumsifia lakini kwa namna alivyoweza kuisimamia timu yake katika gemu mbili za awali hakika anastahili kupongezwa. Simba imecheza vizuri katika mechi zote mbili. Timu imekuwa ikicheza kwa kasi katika mtindo wa kupanga mashambulizi.
Katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Sport, Kerr aliwapaga wachezaji, Hassan Kessy, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murishid na Justice Majabvi katika idara ya ulinzi, Said Ndemla, Awadh Juma, Mwinyi Kazimoto katika eneo la kiungo, Musa Mgosi, Peter Mwalyanzi na Hamis Kiiza katika safu ya mashambulizi.
Safu ya ulinzi haijafanya makosa, Kessy na Tshabalala wameendelea kucheza kwa viwango vya juu katika fullbacks, wakati Juuko ameendelea kujiweka katika orodha ya mabeki bora wa kati katika VPL, Mganda huyo amekuwa akitumia nguvu na akili kiasi cha kumfanya Majabvi kucheza vizuri kama mlinzi wa mwisho katika gemu ya kwanza na hata aliporudi Hassan Isihaka katika gemu ya Mgambo safu ya ulinzi iliendelea kucheza kwa umakini, utulivu na kitendo cha kutoruhusu bao katika dakika 180 ni dalili njema.
Ni dhamira iliyokuwepo, kuchukua alama 6 katika gemu mbili za kwanza tena wakifunga magoli matatu ugenini. Kerr alimuanzisha benchi Kiiza katika mchezo wa jana na nafasi hiyo akacheza Mwinyi. Kutawala mchezo mbele ya Mgambo iliyokuwa na Mohamed Samatta, Helbert Charles na Chande Magoya katikati ya uwanja ni kielelezo kingine kuwa eneo la kati la Simba limeendelea kuimarika lakini bado wana u-haba wa kupiga pasi za mwisho.
DHIDI YA KAGERA SUGAR
Itakuwa mechi ya tatu ya msimu na ya kwanza kwa Simba katika uwanja wa nyumbani (uwanja wa Taifa, Dar es Salaam). Simba wamekuwa wakisisitiza kushinda kila mchezo na kabla ya kuwavaa mahasimu wao Yanga SC wiki ijayo, Kerr atakutana na timu nyingine inayowasumbua sana. Kagera imecheza gemu mbili ugenini, walishinda 1-0 dhidi ya Mbeya City kisha wakapoteza Jumatano hii mbele ya Majimaji FC kwa goli 1-0.
“Historia zimewekwa ili kuvunjwa, tutajitahidi kuhakikisha tunashinda kila
mechi inayokuja mbele yetu”, ni maneno ya mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Simba, Hajji Manara mara baada ya kushuhudia timu yake ikishinda kwa mara ya pili mfululizo. Baada ya kuvunja mwiko wa kutoshinda Tanga kwa misimu mitatu mfululizo, je, Simba wataifunga Kagera Sugar kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2012/13 katika uwanja wa Taifa?
Kwa hisani ya Shafii Blog

No comments:

Post a Comment