Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 17, 2015

NAHODHA WA PRISONS AIPIA MBEYA CITY

 Laurian Mpalile, Nahodha wa kikosi cha Tanzania Prisons 'Wajelajela'
NAHODHA wa Tanzania Prisons, Laurian Mpalile amesema mchezo dhidi ya Mbeya City utakuwa mgumu lakini haiwafanyi  kuogopa kucheza nao.
Mpalile alisema hasira za kufungwa na Yanga wanakwenda kuzimalizia kwa Mbeya City japo wanafahamu ni timu nzuri na inafundishwa na mwalimu mzuri.
“Tumefungwa na Azam FC mabao 2-1, jana (juzi) tumefungwa na Yanga wametufunga mabao 3-0, ni matokeo mabaya kwetu hivyo hasira zetu tutazimalizia kwa Mbeya City japo tunapokutana nao mchezo huwa mgumu”, alisema Mpalile
Pia Mpalile alisema dakika 20 za mwanzo walicheza kwa kuzuia zaidi huku wakitumia nguvu kutokana na maelekezo ya kocha kuona Yanga wanafanya mashambulizi yao kupitia wapi na kusahau kwenda kunashambulia.
Mpalile alimtupia lawama golikipa wao na kusema mabao mawili ya mwanzo walifungwa kutokana na makosa yake lakini wanamheshimu kwa sababu ni makosa ya mchezo ambayo hata mchezaji mwingine anaweza kufanya.
Pia nahodha huyo amekiri kadi nyekundu aliyooneshwa beki wao Josephat ilikuwa sahihi kwa sababu alikuwa ni mchezaji wa mwisho alipomfanyia Msuva  rafu ya nyuma ‘tackling from behind’ akiwa ndani ya eneo la goli
Mpalile pia alisema kubadilisha makocha  kwenye timu inachangia yetu kufanya vibaya kwasababu kila kocha anakuja na falsafa yake hivyo inakuwa vigumu kubadilika haraka kuendana na matakwa ya kocha.

No comments:

Post a Comment