Mchezaji mpya wa Yanga Mzimbabwe Thabani Kamusoko (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja wa Hafidhi Saleh |
HATIMAYE kiungo na nahodha wa
FC Platinum ya Zimbabwe, Thabani Michael
Kamusoko ametua jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kusaini mkataba wa
kujiunga na Yanga.
Kamusoko alipokewa na Meneja
wa Yanga, Hafidh Saleh kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA), ambapo alipelekwa katika kikao na uongozi kwa mazungumzo.
Akizungumza uwanjani hapo
baada ya kutua mchezaji huyo, alisema amekuja kikazi zaidi na Yanga hawatajutia
kumsajili endapo watafikia makubaliano.
Kamusako aliyewahi pia
kuchezea Dynamos FC ya Zimbabwe, anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili wa
kuichezea Yanga.
Mchezaji huyo rasta
aliyeivutia Yanga ilipokutana na FC Platinum katika Kombe la Shirikisho
mwanzoni mwa mwaka huu, anatarajia kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mghana Kpah
Sherman aliyeuzwa Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini.
Lakini pia, Yanga iko mbioni
kuwaacha wachezaji wake wengine wawili wa kigeni, beki Mghana Joseph Tetteh
Zutah na kiungo Mbrazili Andrey Coutinho.
Dirisha la usajili Tanzania
Bara linatarajiwa kufungwa saa 6:00 usiku leo huku ikibaki nafasi ya kuwasajili
wachezaji huru pekee.
Baada ya Yanga kutolewa
katika robo fainali michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame, imekitathmini kikosi chake na kugundua Zuttah na Coutinho hawana faida.
Coutinho alijiunga na Yanga
SC msimu uliopita akiletwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazili mwenzake,
Marcio Maximo na hadi sasa ameichezea timu hiyo mechi 33 na kuifungia mabao
sita.
Mbrazili huyo alikuwa ana
wakati mzuri chini ya kocha Maximo, lakini tangu ujio wa Mholanzi, Hans van der
Pluijm hana namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Zuttah amesajiliwa Juni mwaka
huu kutokana na kupendekezwa na kocha Pluijm, lakini baada ya wiki mbili za
Kombe la Kagame, uongozi umeona hana umuhimu.
Mbali na Sherman, Coutinho na
Zuttah, wachezaji wengine wa kigeni waliopo Yanga ni Mkongo Mbuyu Twite,
Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
Yanga SC ilifungwa kwa
penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika robo fainali ya
Kagame dhidi ya Azam FC wiki iliyopita na tathmini ya baada ya mashindano,
inaonesha timu inahitaji marekebisho kadhaa.
No comments:
Post a Comment