TIMU
ya soka ya Taifa ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanite, imeanza
vibaya mbio za kuwania tiketi ya fainali za Afrika, baada ya jana kufungwa
mabao 4-0 na Zambia Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ilikuwa
huzuni kwa Watanzania wote waliojitokeza Uwanja wa Azam, Chamazi wakiongozwa na
Rais wa TFF, Jamal Malinzi namna ambavyo Tanzanite walivyonyanyaswa na mabinti
wenzao shupavu wa Zambia.
Tanzanite
inayofundishwa na mzalendo, Rogasian Kaijage leo ilizidiwa kabisa na
Shepolopolo Uwanja wa Azam na kujikuta hadi mapumziko ikiwa tayari
imekwishabugizwa 3-0.
Mabao
ya Shepolopolo yalifungwa na Memory Phiri dakika ya nne, Irene Lungu dakika ya
20 na Barbara Banda dakika ya 33.
Kipindi
cha pili, Zambia walirudi na moto wao tena na kufanikiwa kupata bao la nne,
mapema tu dakika ya 50 kwa penalti kupitia kwa Marry Wilombe.
Refa
Batouli Ibrahim wa Sudan alitoa penalti hiyo baada ya Anastazia Anthony
kumfanyia faulo mshambuliaji wa Zambia, Memory Phiri.
Sasa
Tanzanite inatakiwa kwenda kushinda mabao 5-0 ugenini ili kusonga mbele.
Kikosi
cha Tanzanite: Najjiat Abbas, Zuwena Aziz, Happiness Hezron, Maimuna Hamisi,
Anastazia Anthony, Donisia Daniel, Hamisa Athumani, Neema Paulo, Asha Shaaban
Hamza/Janet Cloudy (dk 40), Shelider Boniphace na Stumai Abdallah.
Zambia:
Hezel Natasha Nali, Mary Wilombe/Osala Kaelo (dk 75), Margaret Belemu, Martha
Tembo, Mlika Limwanya, Lwendo Chisamu, Esther Mukwasa, Irene Lungu, Grace
Chanda, Barbara Banda na Memory Phiri/Agnes Musesa (dk 83).
No comments:
Post a Comment