WACHEZAJI wa timu ya Taifa, ‘Taifa
Stars’, Abdi Banda na Mohamed Hussein watakosa mchezo wa marudiano dhidi ya
Uganda utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nakivubo nchini Uganda.
Wachezaji hao ambao ni majeruhi baada ya kuumia kwenye mazoezi hawataweza
kusafiri na timu hivyo nafasi zao zimezibwa na wachezaji wengine ambao wapo
kambini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kocha Mkuu wa Taifa
Stars. Charles Mkwasa alisema kuwa licha ya kuwakosa , Abdi Banda na Mohamed Hussein na Jonas Mkude ambaye alikwenda Afrika
Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio anaamini wachezaji waliopo watacheza
vizuri kwenye mchezo huo wa marudiano wa kutafuta kufuzu fainali za Afrika kwa
wachezaji wa ndani (CHAN)
“Tunashukuru kwa ushirikiano tuliopata
toka kwenu waandishi wa habari na mashabiki hivyo tunawaahidi kufanya kile
ambacho watanzania wengi wanakitazamia japo tutawakosa wachezaji watatu”,
alisema Mkwasa
Pia alisema kipa Mwadini Ally hakuweza
kujiunga na kambi ya timu hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia hivyo naye
hatosafiri
Taifa stars imeondoka nchini jana jioni kuelekea Kampala -
Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes utakaochezwa
Jumamosi ikiwa na wachezaji 20, bechi la
ufundi 7, pamoja na viongozi kwa shirika la ndege la Rwanda (Rwada Airi).
Mchezo wa jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za
Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda, huku mechi
hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo.
Wachezaji
wanaosafiri ni: Ally Mustafa, Mudathir Khamis, Juma Abdul, Shomari Kapombe,
Haji Mngwali, Michael Aidani, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani, Nadir Haroub,
Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla, Saimon Msuva, Deus
Kaseke, Ramadhan Singano, Atupele Green, Rashid Mandawa, John Bocco na Ame
Ally.
Mara baada ya kuteuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Mkwasa alitaja kikosi wachezaji 26 na kuwa nacho kambini kwa wiki moja
huku wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.
Benchi la Ufundi litaongozwa na Mkwasa, Mshauri wake wa
Ufundi, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’, Msaidizi wake Hemed
Morocco, kocha wa makipa, Manyika Peter, Mtunza Vifaa Hussein Swedi ‘Gaga’,
Meneja Omar Kapilima pamoja na Mratibu Msafiri Mgoyi.
Stars
inatakiwa kushinda 4-0 Jumamosi ili kusonga mbele CHAN
No comments:
Post a Comment