Mwenyekili wa kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe na Mjumbe wa kamati ya Utendaji, Collin Frisch wakiondoka kwenye ofisi za TFF baada ya kikao |
Mjumbe wa kamati ya
Utendaji, Collin Frisch (Kushoto) akiongea na Katibu wa Sputanza Said George na mchezaji Ramadhan Singano (kulia) wakiteta baada ya kutoka nje |
KLABU ya Simba imeshindwa na mshambuliaji Ramadhan Singano
‘Messi’ kwenye mgogoro wao wa kimkataba ambao umedumu kwa takribani miezi
mitatu.
Maamuzi ya mgogoro huo yametolewa mbele ya wandishi wa
habari na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Selestine Mwesigwa
na kusema Simba imeshindwa kutekeleza masharti ya mkataba ambayo waliagiza
wakayafanyie kazi lakini hadi kikao cha jana kinakaa hakuna kilichotekelezwa.
“Awali TFF tulimwita Ramadhan Singano na uongozi wa Simba
baada ya kuwasikiliza kila mmoja tukaagiza wakae meza lakini Simba hawakufanya
hivyo na shauri hilo likalazimika kupelekwa kwenye kamati ya Maadili, Sheria na
Hadhi za wachezaji na maamuzi yametoka kuwa mchezaji Ramadhan Singano yupo huru
kuanzia leo”, alisema Mwesigwa.
Mwesigwa alisema Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za
Wachezaji, iliwakilishwa na mwenyekiti Advocate Richard Sinamtwa na mchezaji
Ramadhan Singano alikuwa amefuatana na Mwenyekiti wa Sputanza Mussa
Kisoky na katibu Said George wakati Simba iliwakilishwa na Mwenyekili wa kamati
ya Usajili, Zacharia Hans Poppe na mjumbe wa kamati ya
Utendaji, Collin Frisch na Mkurugenzi wa Wanachama wa TFF, Eliud Mvella
Kikao hicho kichukua saa tano kumalizika huku
kila upande ukilazimika kutolewa nje wakati upande mwingine ukihojiwa mwishoni
upande wa Simba ulitoka ukiwa umenyong’onyea wakati Kisoky na wenzake walitoka wakicheka huku
wakikumbatiana na kuwadokeza waandishi kuwa “Tumeshinda kijana yupo huru ila
sisi si wasemaji subirini TFF watatoa taarifa kamili”
Baadae gazeti hili lilimtafuta Mwenyekiti wa
kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na kuweka wazi kuwa
hawajaridhishwa na maamuzi ya kamati hiyo hivyo watakutana ili kujua hatua
zaidi za kuchukua ikiwezekana watakata rufaa kwenye kamati ya Usuluhishi ya
mambo ya michezo (CAS) ambayo ipo chini ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni
(FIFA).
“Tuliwasilisha ushahidi wote mbele ya Kamati, tumeonyesha
mshahara wake ulikuwa kiasi gani na tumeonyesha kwa nini alikuwa anapewa laki
moja (100,000) zaidi.
Ili akalipie kodi ya nyumba, lakini bado hatukueleweka. Tunaamini hapa si mwisho, vipo vyombo vingine ambavyo vitatupa haki yetu, tunakwenda kukutana kuangalia uwezekano wa kulipeleka suala hili huko
Ili akalipie kodi ya nyumba, lakini bado hatukueleweka. Tunaamini hapa si mwisho, vipo vyombo vingine ambavyo vitatupa haki yetu, tunakwenda kukutana kuangalia uwezekano wa kulipeleka suala hili huko
Kamati ya
Sinamtwa imejiridhisha Messi hakuwahi kupewa nyuma ya kuishi na Simba jambo
ambalo ni kinyume cha Mkataba baina yake na klabu hiyo hivyo imemevunja rasm,I
mkataba wake na kusema yupo huru kusajiliwa na klabu yoyote.
Messi
alikuwa analalamikia Simba kupeleka TFF mkataba wa miaka mitatu wakati yeye
alikuwa na mkataba wa miaka miwili na Simba jambo lililoleta utata hadi
Sputanza kuamua kumsaidia na hatimaye Messi ameshinda.
Messi
alisajiliwa Simba miaka minne iliyopita kwenye Simba B na baadae kuingiwa
kwenye kikosi A baada ya uwezo wake kuwaridhisha makocha mbalimbali ambao
wamekuwa wakiifundisha Simba kwa nyakati tofauti
No comments:
Post a Comment