KATIKA hali
ambayo ni nadra kutokea timu za Simba na Azam FC, leo zimejikuta zikikutana kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar
es Salaam.
Azam FC ambao
wananolewa na Stewart Hall ndio walikuwa wa kwanza kufika eneo hilo na kuanza
mazoezi kama programu ya kocha ilivyopanga na baadae Simba nayo iliwasili eneo
hilo na kuanza mazoezi chini ya kocha wao mwingereza Dylan Kerr.
Azam walikuwa
upande wa kushoto wakifanya mazoezi ya stamina huku Simba wao walikaa kulia na
kuanza mazoezi yao lakini kutokana na ufinyu wa eneo Simba walilazimika
kukimbia na kupita eneo ambalo Azam walikuwa wakifanya na kuwafanya wachezaji
kuanza kutaniana maana wote walikuwa wakikimbia kuelekea upande mmoja lakini
Simba walienda mbali zaidi ya Azam.
Kocha Kerr alikuwa akiongoza mazoezi kwa vitendo
alisikika akiwaambia kuwa waweke mawazo yao kwenye Simba na siyo kufikiria
Azam, Yanga au Ruvu shooting bali ni Simba kwanza.
Zoezi la Simba
kuendelea kufanya mazoezi kupita eneo ambalo Azam FC walipo na sasa ikamfanya
Mgosi kujisahau na kuanza kupiga stori na mchezaji wa Azam FC hadi alipoitwa na
kocha Matola kwani kocha alikuwa bado anaendelea na program ya mazoezi
Wakati Simba na
Azam FC wakiwa Coco, wapinzani wao Yanga wao walikuwa Ufukwe wa Gymkhana
wakifanya mazoezi.
Simba inayonolewa
na Dylan Kerr inajiandaa na ligi kuu inayotarajiwa kuanza Agosti 22 wakati Azam
na Yanga wao wanajiandaa na mashindano ya Kagame yanayotarajiwa kuanza Julai 18
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment