KIPA Angban
Vincent de Paul amewasili jijini Dar es
Salaam juzi na jana amefanya mazoezi mepesi mepesi kwenye ufukwe wa Coco akiwa
na Wawa Sergio wakati wenzake wakijinoa vilivyo chini ya kocha Mkuu Stewart
Hall.
Angban amekuja Azam FC kwa ajili ya kusaini mkataba wa
kujiunga na timu hiyo baada ya kuwepo kwa mazungumzo kabla ya kutua nchini.
Kipa huyo mzaliwa wa Ivory Coast Ivory ametokea klabu ya
Jeunesse ambayo inashiriki ligi kuu ya
kwao, aliwasili jana wachezaji wengine wawili wa Azam FC raia wa Ivory Coast,
beki Serge Wawa Pascal na mshambuliaji Kipre Tchetche.
Akizungumza jijini, Kocha
Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall alisema kuwa anashukuru ujio wa kipa huyo
na kusema kabla ya kusaini itabidi awe amefanya majaribio ili kujiridhisha na
kiwango chake.
“Ni kweli amekuja Azam ila yupo kwa majaribio endapo
atafuzu basi atasaini mkataba ili aaanze kutumikia klabu’, alisema Hall
Katika mazoezi ya jana Angban, Wawa na Kipre Tchetche
walifanya mazoezi yao pekee kwavile walichelewa ili kutafuta kasi ya kuendana
na wenzao ambao walishaanza mazoezi mmoja uliopita.
Azam FC
inamchukua kipa huyo kwa lengo la kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano
ya Afrika kwani mwakani itacheza Kombe la Shirikisho.
Endapo atasani Azam FC, kipa huyo atakwenda kugombea namba na makipa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ali.
Usajili wake ukikamilika, Azam itakuwa na wachezaji wanne kutoka Ivory Coast, wengine ni Serge Wawa Pascal na pacha, Kipre Herman Tcheche na Kipre Michael Balou.
Endapo atasani Azam FC, kipa huyo atakwenda kugombea namba na makipa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ali.
Usajili wake ukikamilika, Azam itakuwa na wachezaji wanne kutoka Ivory Coast, wengine ni Serge Wawa Pascal na pacha, Kipre Herman Tcheche na Kipre Michael Balou.
Angban alizaliwa Februari 2, 1985 mjini Anyama, Ivory Coast
amewahi kudakia timu ya Taifa ya vijana
chini ya U-20 ya Ivory Coast katika fainali za Afrika zilizofanyika Benin mwaka
2005 pia aliiwakilisha nchi yake katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008.
Amewahi kudakia timu ya Taifa ya wakubwa ya Ivory Coast ‘Tembo’ katika michuano ya CHAN ikiwemo ile ya mwaka 2009, ambapo Tanzania ilicheza nao na kushinda bao 1-0, lililofungwa na Mrisho Ngassa, langoni akiwa yeye.
Angban aliibukia
katika klabu ya vijana ya Rio Sport d'Anyama kabla ya kupandishwa kikosi cha
kwanza mwaka 2005, na timu za Sewe Sports, ASEC Mimose kabla ya kwenda kuchezea timu ya vijana
ya Chelsea chini ya U-20.
No comments:
Post a Comment