Wenyeji Chile wametwaa Taji lao la
kwanza kabisa baada ya kuibwaga Argentina kwa Penati 4-1 kufuatia Sare
ya 0-0 katika Dakika 120 za Fainali ya Copa America, Kombe la Mataifa ya
Marekani ya Kusini, iliyochezwa mbele ya Halaiki ya Mashabiki ndani ya
Estadio Nacional Santiago Jijini Santiago. Kipigo hiki kimeendeleza ukame wa
Argentina wa Miaka 22 wa kutotwaa Taji lolote tangu walipobeba Copa
America Mwaka 1993 huko Ecuador na pia unamfanya Kepteni wao Lionel
Messi, aliewahi kuwa Mchezaji Bora Duniani mara 4, aendelee kutokuwa na
mafanikio yeyote na Le Albiceleste tofauti na akiwa na Klabu yake FC
Barcelona ya Spain.
Kwa Chile, ushindi huu umemaliza Karne
yao ya kushiriki Mashindano bila Taji lolote baada ya kufanikiwa kufika
Fainali 4 za Copa America, zile za 1955, 1956, 1979 na 1987, na kufungwa
zote.
Chile,
chini ya Kocha toka Argentina Jorge Sampaoli, hawakucheza Soka la
kuvutia na walikosa nafasi moja ya wazi katika Dakika za Nyongeza 30
wakati Argentina, chini ya Kocha Gerardo 'Tata' Martino, nao walikosa
nafasi ya wazi wakati Gonzalo Higuain alipokosa ndani ya Dakika 90.
Ushindi! 4-1 kwa mikwaju ya penati

Balaa!! Alexis Sanchez alipowafungia mkwaju wa Ushindi

Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuitoa Argentina

Mikwaju ya penati ikiendelea..


Kipa wa Chile Claudio bravo akiwa amebeba juu zawadi yake ya Golden Grove

Eduardo Vargas akiwa na mwanae pamoja na Tuzo yake


TASWIRA

Dakika 120 zilimalizika bila kufungana tena kwa kutoka 0-0 na mikwaju ya penati kupigwa!

Dakika 90 zilimalizika bila kufungana na kuongezwa muda wa dakika 30!

Angel Di Maria akubali yaishe mapema kipindi cha kwanza! Lavezzi alichukuwa nafasi yake

Kipindi cha pili kinaendelea..

Mashabiki wenyeji chile!
VIKOSI:
Argentina Wanaoanza: Romero, Zabaleta, Demichelis, Otamendi, Rojo, Biglia, Mascherano, Pastore, Messi, Aguero, Di Maria
Chile wanaoanza: Bravo, Isla, Medel, Silva, Beausejour, Aranguiz, Diaz, Vidal, Valdivia, Sanchez, Vargas
No comments:
Post a Comment