Kwa
kuzingatia marekebisho ya Kanuni ya Ligi Daraja la Pili (SDL)
yaliyofanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) hivi karibuni, SDL kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa
katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na
ugenini.
Timu
itakayoongoza kundi itacheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa
2016/2017 wakati ya mwisho katika kila kundi itarudi kucheza Ligi ya
Mkoa wake kwa msimu wa 2016/2017.
Makundi
ya SDL ni kama ifuatavyo; Kundi A ni Abajalo FC (Tabora), Singida
United (Singida), Mvuvuma FC (Kigoma), Milambo FC (Tabora), Green
Warriors (Dar es Salaam) na Transit Camp (Dar es Salaam).
Timu
zinazounda kundi B ni Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma (Mara),
Pamba FC (Mwanza), AFC Arusha, Madini FC (Arusha) na Alliance Schools
(Mwanza).
Kundi
C ni Kariakoo (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar
es Salaam), Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers (Dar es
Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).
Nazo
African Wanderers (Iringa), Mkamba Rangers (Morogoro), Town Small Boys
(Ruvuma), Wenda FC (Mbeya), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya) na Sabasaba
United (Morogoro) zitakuwa kundi D.
Klabu
nyingi bado hazijatuma jina la uwanja wa nyumbani, hivyo zinakumbushwa
kufanya hivyo haraka ili kurahisisha upangaji wa ratiba.
Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016 inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment