MTOTO HUYU ANATAFUTWA NA HIMID MAO WA AZAM FC
Picha hiyo iliambatana maneno
yafuatayo: “My favorite picture for today (picha yangu bora kwa leo)
mwenye mtoto huyu huyu anitafute nina zawadi yake”, mwisho wa kumnukuu
Mao.
Wachezaji wa Azam wameonekana
kufurahia kuitupa nje timu ya Yanga ambayo imekuwa ikiwapa tabu pindi
wanapokutana na historia inaonesha Azam na Yanga zinapokutana basi mara
nyingi Yanga huibuka na ushindi.
Kwenye mchezo huo, Mao alicheza
kwa dakika zote 90 na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopiga penati
ambapo yeye alipiga penati ya tatu na kufunga.
Mao anamtafuta mtoto huyo ili
ampe zawadi japo hajaitaja ni zawadi gani, kwa mtu yeyote anayemfahamu
mtoto huyo, wazazi wake au mtu wa karibu na mtoto huyo basi anaweza
kutoa taarifa kwa watu hao ili wawasiliane na Mao ili waweze kupatiwa
zawadi hiyo.
Post a Comment