SIMBA itaondoka
jijini kesho alfajiri kwenda kuweka kambi kwenye safu za milima ya Lushoto mkoani
Tanga kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti
22.
Akizungumza
baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye Ufukwe wa Coco, jana, Kocha Mkuu wa
Simba, Dylan Kerr alisema wanakwenda kuweka kambi kwa wiki mbili Lushoto kwa
sababu ya hali ya huko ni nzuri kwa mazoezi.
“Kwa sababu
hali ya hewa ya Lushoto ni baridi itafanya wachezaji wafanye mazoezi sana
kuliko hali ya hewa ya joto pia itasaidia kocha wa fitness, Dusan kujua stamina
(fitness) ya kila mchezaji na saikolojia”,
alisema Kerr.
Pia Kerr
alisema anafurahi kwa sababu muitikio wa wachezaji ni mzuri japo amepata taarifa kuwa kuna wengine ambao
wapo kwenye mfungo wa Ramadhan lakini hakuna tofauti kati yao.
Kerr alisema
baada ya kambi ya Lushoto ataomba apate mechi tano za kirafiki ili apime
stamina (fitness) na kile ambacho amefundisha kwa wiki tatu
Wachezaji
watakaondoka ni kipa Ivo Mapunda ambaye ni chaguo la kocha wa makipa, Idd Abdul
ambaye amemalizana na uongozi juzi kutokana na pendekezo la kocha huyo kwani
uongozi ulikuwa unasusua umsajili nani kati ya Ivo na Kaseja.
Wengine ni kipa
Peter Manyika, Denis Richard, Samir
Nuhu, Mohamed Fakhi, Murushid Juuko, Peter Mwalyaje, Musa Hassan ‘Mgosi’, Elias
Maguri, Awadh Juma, Ibrahim Ajib na Emanuel Alex ambaye anafanya majaribio
akitokea Afrika Kusini katika klabu ya Olmpio inayoshiriki ligi daraja la pili.
Pia wapo Issa
Abdallah, Said Issa Mbaraka Yusuf na David Kisu ambao wamepandishwa kutoka
kwenye timu B.
No comments:
Post a Comment