Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi
matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mfuko
huo wa makundi matatu umetokana na marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) yaliyofanywa hivi karibuni na Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao cake
kilichofanyika mjini Zanzibar.
Timu ya kwanza katika kila kundi
la ligi hiyo itakayoanza Septemba 12 mwaka huu itapanda kucheza Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) kwa msimu wa 2016/2017 wakati timu itakayoshika nafasi
ya mwisho katika kila kundi itashuka kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL)
kwa msimu wa 2016/2017.
Kundi A linaundwa na timu za African Lyon
FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers
FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal
Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam
na Polisi Dodoma.
Timu zinazounda kundi B ni Burkina Faso FC
(Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC
(Iringa), Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting
(Pwani).
Kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC
(Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC
(Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).
No comments:
Post a Comment