Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika - CAF limewateua waamuzi wa kike kutoka Tanzania kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake U-20 mwaka 2016 kati ya Congo DR dhidi ya Gabon.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa jumamosi tarehe 09.05.2015 jijini Kinshasa - Condo DR, mwamuzi wa kati ni Jonesia Rukya, akisaidiwa na washika vibendera Dalila Jafari na Sophia Mtongoli huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma.
Wakati huo huo Elizabeth Kalinga ameteuliwa kuwa kamisaa wa mchezo kati ya Kenya dhidi ya Botswana kuwania kufuzu kwa michuani ya Olympiki, mchezo utakaofanyika Mei 31, 2015 nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment