Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, April 3, 2015

WAJUE MABONDIA WA TIMU YA TAIFA WATAKAOWAKILISHA NCHINI KWENYE MASHINDANO YA KIMATAIFA

Picture 001 










                                                                                                         April 2, 2015

Taarifa kwa vyombo vya habari

        Yah:- Timu ya Taifa ya Ngumi 2015.

Hatimaye baada ya mchakato wa muda mrefu,  uliofanyika kwa umakini kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa hatimaye Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limepata wachezaji wa timu ya Taifa ya Ngumi 2015. Katika mashindano ya kimataifa  yaliyoshirikisha timu za taifa kutoka Uganda na Kenya, mashindano yaliyomalizika kwa mafanikio, Jumamosi ya tarehe 28.03.2015 uwanja wa Taifa wa ndani .
Mabondia waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa katika timu zao zinafanyika na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa kuanza mazoezi kabla ya tarehe 15.04.2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hasa mashindano  ya Michezo ya Afrika (All African Games) Septemba 4-19. Brazzaville Congo. Na mashindano ya Ubingwa wa Dunia (AIBA World Boxing Championships) Octoba 5-18 Doha Qatar.
Mabondia waliochaguliwa kwa uzito wao ni kama ifuatavyo:-

49 kgs L/FLY
·         Mohamed Mzeru –JKT
·         Maulid Athumani-
·         Ibrahim Abdalah – Magereza.
52 Kgs Fly Weight.
·         Juma Ramadhani- Temeke
·         Said Hofu- JKT
56 Kgs Bantam Weight
·         Ahamad Furahisha- JKT
·         Bon Mlingwa- JKT
60 Kgs Light weight.
·         Elias Mkomwa- JKT
·         Bosco Bakari- JKT
·         Fabian Gaudence- NGOME
64 Kgs Light Weight

·         Kassim Mbwitike- JKT
69 Kgs. Welter Weight.
·         Said Gulushad – JKT
·         Seleman Bamtulah- JKT
75 Kgs Middle Weight.
·         Ivan Mussa – Kagera
81 Kgs light Heavy
·         Hamidu Halfan-JKT
91 Kgs Heavy weight
·         Alex Sitta- JKT
·         Nuru Ibrahim- Magereza
Aidha BFT  inawapongeza Mabondia wote kwa jitihada kubwa walizofanya na hatimae kuchaguliwa kuwa mabondia wa timu ya taifa ya ngumi 2015.

Nakala kwenu kwa  Taarifa.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu (BFT)







No comments:

Post a Comment