“SIKU hizi sisi tunakwenda na idadi ya siku tu hivyo kesho tunatarajia mabao 12” Hayo ni maneno ya Kocha msaidizi wa Yanga, Charles
Boniface Mkwasa aliyokuwa akimwambia Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka
Nchini (TFF) Salum Madadi alipokuja kumsalimia
wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume zilipo ofisi za TFF.
Kauli hiyo ilikuja baada ya Madadi kumtania Mkwasa
akimwambia juzi tarehe 8 mlishinda mabao maneno dhidi ya Coastal Union na kesho
tarehe 12 tutarajie nini? Ndipo Mkwasa alipomjibu siku hizi sisi tunakufunga
kwa idadi ya tarehe ya siku husika hivyo kesho (leo) tunafunga mabao 12 na
kuachia kicheko kilichofuatiwa na kugongeana mikono.
Yanga imegeuka gumzo baada ya kuifunga Coastal Union ya
Tanga mabao 8-0 kwenye mchezo uliopita ambao ulichezwa Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam na kufanikiwa kuendelea kukaa kileleni ikiwa na pointi 43 baada
ya kucheza mechi 19, pointi sita mbele ya mabingwa watetezi Azam FC wanaoshika
nafasi ya pili.
Yanga leo asubuhi walifanya mazoezi mwisho kujiandaa na
mchezo wao na Mbeya City kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kuvuta
idadi kubwa ya watazamaji kama vile kuna mechi muda huu kwani walikuwa
wakishangilia.
Wachezaji wa Yanga walionekana kuwa morali ipo juu na hakuna
wanachohofia kwani kila mchezaji alionekena kufanya vizuri kwenye mazoezi hayo.
Wachezaji Juma Abdul na Dany Mrwanda walifanya mazoezi
mepesi mepesi peke yao lakini Jerryson Tegete yeye hakufanya mazoezi kabisa
kutokana na kuwa majeruhi muda mrefu.
No comments:
Post a Comment