Na Andrew Chale wa Modewji blog
Kitu
kingine kwa mwanamuziki anayefaanya vizuri Bongo nan je ya Bongo, Nasib
Abdul maalufu kama Diamond Platinumz, ameweza kuibuka nacho ni suala
la kuisaidia jamii ya wakazi wa Tandale, eneo alilozaliwa na kukulia
katika maisha yake.
Katika
kurasa wake wa Instagram, Diamond Platinumz ama pia akifahamika kama
Chibu Dangote, alitupia picha kadhaa alipokuwa katika ofisi za Edgepoit
Company Ltd huku akishukuru kwa kupatiwa Bima 200 za Afya kwa wakazi
waTandale.
Kwa
mujibu wa maelezo hayo, Diamond alibainisha kuwa, kampuni hiyo
wamewezesha upatikanaji wa Bima ya Afya kwa wakazi 200 wa Tandale. Bima
hiyo ya Afya, ni ya mwaka mmoja ambayo itawawezesha wakazi hao
watakaopatiwa bima hiyo kupata huduma katika Hospitali mbalimbali
nchini.
Diamond akiwa katika picha ya pamoja na mafisa wa Edge Point Comapany Ltd, alipotembelea ofisi hizo
Bima
ya Afya inajishughulisha na utoaji wa bima ya afya kwa watu wote
ikiwemo ya watu wa maisha ya kati na wasio katika ajira rasmi. Huku kwa
wanaotaka kujiunga wanaweza kupiga *150*57# au 0714821422 au 0755885515.
Diamond
ni kati ya wasanii wakubwa ambaye mara zote amekuwa mstari wa mbele
kuisaidia jamii hasa katika makazi aliyokulia ya Tandale ambayo mara
nyingi kutokana na namna ya mazingira yake watu wengi ukiwaelezea
Tandale wametokea kutokupapatia thamani lakini Diamond amekuwa
akiheshimika na kutoa sifa mbalimbali ya maeneo hayo ya Tandale bila
kuficha kama wafanyavyo wasanii wengine wanaojipa sifa za kuishi maeneo
ya kitajili ikiwemo Masaki, Mbezi na Mikocheni.
Unapojiunga na bimaAFYA unakuwa na nafasi ya kupatiwa huduma bure katika hospitali mbalimbali karibu nchi nzima.
KWA HISANI YA MO BLOG
No comments:
Post a Comment