
Kwa Nchi za Afrika, Algeria ndio ipo juu ikiwa Nafasi ya 18 ikifuatiwa na Ivory Coast walio Nafasi ya 20.
Italy wameingia 10 Bora kwa mara ya kwanza tangu Juni 2014 na kuwaporomosha Mabingwa wa Dunia wa zamani Spain ambao sasa wako Nafasi ya 11.
Listi nyingine ya Ubora Duniani itatolewa hapo Aprili 9.
1. Germany
2. Argentina
3. Colombia
4. Belgium
5. Netherlands
6. Brazil
7. Portugal
8. France
9. Uruguay
10. Italy
Maeneo ya Tanzania:
96 Oman
97 Iraq
98 Belarus
99 Saudi Arabia
100 Tanzania
101 Jordan
102 Antigua and Barbuda
102 Ethiopia
Sare ya bao
1-1 iliyopata Tanzania dhidi ya Rwanda kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa
uliochezwa jijini Mwanza imeisaidia kupanda kwa nafasi saba kwenye ubora wa
viwango ambayo hutolewa na shirikisho la Soka Dunia (FIFA)
Kabla ya
mchezo huo ambao ulikuwa ni kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Tanzania ilikuwa ikishika
nafasi ya 107 lakini msimamo uliotolewa jana inashika nafasi ya 100.
Taarifa hiyo
ambayo ipo kwenye wavuti ya FIFA inasema Nchi za Afrika ambazo zinashika nafasi
za juu ni Algeria ambayo ni ya 18 ikifuatiwa na Ivory Coast ambayo ipo nafasi
ya 20.
Nafasi ya
kwanza imeemnelea kushikiliwa na Ujerumani, ambao ndio mabingwa wa dunia nafasi
ya pili ikishikiliwa na Agentina huku nafasi ya tatu ikienda kwa Colombia
Italy
wameingia kwenye 10 ya dunia bora kwa mara ya kwanza tangu Juni 2014 na
kuwaporomosha Hispania (Spain) ambao sasa wako nafasi ya 11.
Viwango vingine vya ubora vinatarajia kutolewa Aprili 9 mwaka huu
No comments:
Post a Comment