Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 13, 2015

POLISI MORO YAMTIMUA ADOLF RISHAARD



TIMU ya Polisi Morogoro imekatisha mkataba na kocha wake Mkuu, Mohamed Adolph Rishaard kutokana na timu hiyo kucheza chini ya kiwango na kupoteza michezo kwenye ligi Kuu..

Akizungumza  kwa njia ya simu Mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro, Zuberi Chambera alisema kuwa kocha, Mohamed Adolph Richard amesitisha mkataba  naye wa kuifundisha timu kutokana na kufanya vibaya na kusema maamuzi hayo yakifikiwa na kikao cha kamati ya utendaji ya timu.

“Ni kweli kocha wetu Mohamed Adolph Rishard amesimamishwa kufundisha kutokana na sababu zilizotolewa na kupitishwa na kamati tendaji ni baada ya kucheza chini ya kiwango tofauti na makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkataba wetu”, alisema Chembera.

Polisi Moro imepoteza michezo minne, imetoka sare nane na kushinda michezo minne ya ligi kuu Tanzania bara na sasa timu ipo itanolewa na kocha msaidizi, John Tamba wakati wakisaka kocha mkuu mwenye sifa za kufundisha.

Naye Mohamed Rishard alisema kuwa kusitishiwa mkataba wake amelipokea kwa mikono miwili kutokana na timu kufanya vibaya kwani lilikuwepo moja ya kipengele kwenye mkataba kilitamka wazi endapo timu ingepoteza michezo mitatu kamati itamwita na kumhoji na wametekeleza kipengeleza

 “Ni kweli mkataba wangu wa kuifundisha Polisi Moro  umesitishwa kutokana na timu kufanya vibaya na nimeitwa na kamati utendaji na kuhojiwa kwanini timu inafanya vibaya nami nimejieleza lakini kamati hiyo imefikia uamuzi wa kunisimamisha kazi na nimekubaliana nao”, alisema Adolf.

Michezo ambayo Polisi Moro ilipoteza mfululizo  Simba ambayo walifungwa mabao 2-0, Kagera Sugar bao 1-0 na Mtibwa Sugar ambao waliilaza kwa mabao 2-1.

Pia Adolph alitoa tahadhari kwa kocha atayeridhi nafasi yake kujenga falsafa iliyo bora ili aivushe timu  ili isishuke daraja maana yeye aliikuta timu ikiwa  ina pointi nne na yeye amefikisha pointi  ambazo haziwezi kuiondoa kwenye kushuka daraja  na imebaki na michezo nane.

Kocha Mohamed Adolph Rishard alijiunga na klabu ya Polisi Moro wakati timu hiyo ikiwa ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa pili msimu wa mwaka 2013/2014 na kushuka daraja kabla ya kurejea tena ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2014/2015.

No comments:

Post a Comment