MSHAMBULIAJI
Danny Mrwanda wa Yanga anazalimika kukosa mchezo wa dhidi ya Platinum ya
Zambabwe utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
hii.
Akizungumza
jijini Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro alisema kwamba,
Mrwanda alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa marudiano wa Kombe la
Shirikisho dhidi ya BDF XI nchini Botswana, hivyo hatacheza Jumapili.
“Mrwanda
kwenye mchezo dhidi ya BDF XI nchini Botswana alionyeshwa kadi nyekundu hivyo
atakuwa natumikia adhabu hiyo ndio maana hajaingia kambini”, alisema Muro
Yanga SC itamenyana na Platinum FC Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza, raundi ya kwanza ya Kombe la Shrikisho Afrika hivyo Mrwanda atakuwa jukwaani.
Muro amesema Mrwanda amepewa ruhusa maalum ya kutokuwa kambini, ili akamsaidie mke wake kwa sababu amejifungua.
Awali kulikuwepo na tetesi kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC amesimamishwa kwa madai alicheza chini ya kiwango baada ya timu yake kufungwa na Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliochezwa jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

Mrwanda
alishindwa kuifungia Yanga bao la wazi dakika ya 28, baada ya kupewa pasi nzuri
na Simon Msuva, lakini akazubaa na mpira ndani ya eneo la penati hadi akapokonywa
na Juuko Murushid.
Tukio hilo
lilimkera kocha Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ambaye alimtoa na nafasi
yake kuchukuliwa na Hussein Javu
No comments:
Post a Comment