Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 5, 2015

ASHLEY YONG AIPA USHINDI UNITED UGENINI MANCHESTER UNITED KWA KUIFUNGA NEWCASTLE UNITED BAO 1-0


Ashley Young aliipa Ushindi Man United katika dakika za lala salama dakika ya 89 na kufanya 1-0 dhidi ya Newcastle United.Bao tamu la ushindi dakika za mwishoni..na Hapa wachezaji wa Man United wakipongezana
Bao la Dakika ya 89 la Ashley Young limewapa ushindi wa Bao 1-0 Manchester United waliokuwa wakicheza Ugenini huko Saint James Park dhidi ya Newcastle.
Bao hilo lilitokana na makosa ya Kipa wa Newcastle Tim Krul kushindwa kuiondoa Pasi aliyopewa na Mchezaji wake Mehdi Abeid na badala yake kumruhusu Young kuunasa Mpira na kufunga vizuri.
Ushindi huu umewabakiza Man United Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Arsenal ambao wako Nafasi ya 3.
1-0 dakika ya 89 Young anamaliza mchezo kwa bao la ushindi
Young baada ya kumaliza mchezo kwa kuipa ushindi Man United!Rooney akimpongeza Young1-0Ashley Young akiachia shuti na kumfunga kipa wa Newcastle kwenye Uwanja St. James Park
VIKOSI:
Newcastle:
Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Ryan Taylor, Obertan, Abeid, Sissoko, Ameobi, Cisse, Riviere.
Akiba: Anita, Gouffran, Perez, Gutierrez, Armstrong, Satka, Woodman.
Man United: De Gea, Valencia, Smalling, Evans, Rojo, Ander Herrera, Blind, Di Maria, Rooney, Young, Fellaini.
Akiba: Jones, Mata, Falcao, Januzaj, Lindegaard, Carrick, McNair.
Refa: Anthony Taylor

No comments:

Post a Comment