JKT Ruvu |
Red Arrows |
Benchi la Ufundi JKT Ruvu |
Kushoto ni beki wa JKT Ruvu, Damas Makwaya akimzuia Ngoma Patrick wa Red Arrows ya Zambia kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Uwanja wa Karume jini Dar es Salaam na timu kutoka sare ya 0-0 |
TIMU ya Red Arrows ya Zambia imelazimishwa sare ya bila
kufungana na JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam jana.
Red Arrows ambayo inamilikiwa na jeshi ilijikuta ikikubali
sare hiyo toka kwa wanajeshi wenzao wanaonolewa na kocha Minziro.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kumsoma
mpinzani wake ulinogeshwa na pasizilizojaa ufundi na macho na kufanya dakika 45
kuonekana chache.
Kipindi cha
pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambayo yalizidisha kasi ya
mchezo lakini shukrani kwa mabeki wa timu zote kuwa imara na kufanya mpira
uchezwe katikati kipindi chote cha pili
Red Arrows
walionekana kujaribu kucheza shambulizi la haraka (counter attack) lakini
mabeki wa JKT Ruvu walikuwa makini kuvunja mitego ya kuotea.
Baada ya
mchezo huo kocha wa Red Arrows Mathew Phiri, alisema JKT Ruvu ni timu nzuri
kwani hawachoki upesi na wachezaji ni wepesi kusoma mchezo jambo lililowafanya
kushindwa kupenya ngome yao.
“Wapinzani
wetu wa leo ni wepesi kusoma mchezo hivyo imekuwa rahisi kutubana tusiwafunge
lakini pia wana nguvu na pumzi kuweza kuhimili dakika 90 bila kuchoka””,
alisema Phiri
Naye kocha
wa Kiluvya FC, Minziro alisema wachezaji wake wamecheza vizuri lakini hakuacha
kuwasifia wapinzani wao kuwa wapo viziri kwenye utimamu wa mwili (physic) na
kuongeza kuwa mchezo huo ni maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Machi 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Azam Complex jijini Dar es Salaam
Red Arrows
kwenye mchezo wa awali iliifunga Kiluvya FC mabao 3-0 na ikafuatia kuifunga
Ruvu Shooting bao 1-0 na jana kukubali suluhu.
Red Arrows
wameondoka nchini jana baada ya kuweka kambi ya siku kumi kwa ajili ya
maandalizi ya Ligi Kuu ya Zambia inayotarajiwa kuanza Machi mwaka huu ambapo
msimu uliopita ilimaliza ligi ikishika nafasi ya saba sawa na JKT Ruvu ilipo
kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment