Nchini Tanzania si
jambo la ajabu kuona Watoto na wakubwa wakicheza sarakasi mitaani.lakini
sifa hii ya kuwa nchi maarufu kwa sarakasi barani Afrika inatoka wapi,
Mwandishi wa BBC alizuru Dar es Salaam kubaini hayo.
Mcheza
sarakasi Raia wa Zimbabwe Winston Ruddel alianza kusaka vipaji kwa
ajili ya taasisi yake iitwayo Mama Afrika, kituo chake cha kwanza
kilikua jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania, huko alianzisha shule ya
Sarakasi, Mama Afrika
''Awali
ilikua kama nilifanya makosa'', anaeleza Ruddel.'' nilipewa Mkataba
mjini Las Vegas kwa ajili ya maonyesho ya sarakasi, hivyo nikaja
Tanzania kutafuta vijana walio na ufahamu na mchezo wa sarakasi,
tukafanya kazi pamoja, lakini wamarekani hawakuvutiwa na vijana wale.
Tayari nilishawaahidi mkataba, hivyo nikaanza kuwatafutia
kazi.,wishowe,tulipata kazi nyingi zilizonilazimu kufungua shule ili
kukidhi mahitaji.ilianza kwa kosa dogo lililozaa mafanikio makubwa''.
Mmoja
kati ya waliofundisha katika shule hiyo, Selemani Mohamedi Nomondo,
anasema ''nilianza kunyonganyonga viungo vyangu nikiwa na umri wa miaka
mitatu, ikiwa utaanza mapema zaidi, mwili wako utazoea na hutasikia
maumivu, kwa kutazama inaonekana ngumu, kuliko uhalisia ulivyo''.
Maonyesho
ya Mama Afrika hutumia muziki katika kazi zake jukwaani, pia shuleni
wakati wa mafunzo. Ngoma ni kiini cha mchezo wa sarakasi huwapa wasanii
ari ya mchezo na kusaidia katika uchezaji kwa wanakikundi.
Rajab
Zubwa anasema yeye ni mtu wa kwanza kuwa mwanasarakasi '' nilisoma kwa
miaka minne nchini China miaka ya 1960.Tanzania na China walikuwa na
uhusiano wa karibu wa kisiasa hivyo Serikali zote mbili zilianzisha
mafunzo ya kubadilishana, anaeleza'' nilipata faida kubwa nilipokuwa
kwenye shule ya Sarakasi na niliporejea nilikuwa mwalimu wa sarakasi.
Maonyesho
ya Mama Afrika mpaka sasa yamefanyika katika mabara matano, ikiwemo
mjini New York.kuna maonyesho mengi yanafanyika kwa wakati mmoja ,
lakini sio rahisi kuwa sehemu ya maonyesho ni wahitimu wanye uwezo wa
juu pekee kutoka kwenye shule hiyo hufanikiwa kufika katika hatua ya
kimataifa.
Watoto wanakaribishwa katika shule ya Mama Afrika wakati wa mwisho wa wiki na wanapokua likizo.
Tangu
shule hii ilipoanzishwa mwaka 2003 zaidi ya wanafunzi 300 walimaliza
masomo yao.wengi walianza kufanya maonyesho mbali mbali ya sarakasi,
wengine walijiunga na Kampuni za sarakasi duniani.
Pamoja
na tamaduni za micheo hii nchini Tanzania, programu za shule
hazidhaminiwi na Serikali wala Sekta binafsi, shule ya Ruddel iko maeneo
ya Magomeni moja ya eneo waishio watu wengi wa kipato cha chini jijini
Dar es Salaam, baada ya kazi ngumu ya mafunzo wanafunzi hupata chakula.
''Jina
langu Tumaini, mimi ni Mshonaji nguo wa Mama Afrika.huwa tunavaa nguo
halisi za kiafrika jukwaani, tunatumia vitambaa vizuri ambavyo huvaliwa
mitaani.
Naitwa
Deborah Dixon ni mmoja kati ya wasichana wachache ambao hufanya
sarakasi kwa mtindo wa kukunjakunja viungo.wasichana wengi hupenda
kufanya sarakasi kwa mchezo wa kucheza ngoma kwa sababu ya tamaduni za
kifamilia si sawa kwa watoto wao wa kike kutanua miguu na kugalagala
kwenye sakafu.kwa upande wangu kukunjakunja viungo ni sanaa .
Ally
Kibwana Ally anasema'' kwangu mimi kuwa na Mama Afrika kunamaanisha
kuwa niliweza kuishi kutegemea kipaji changu. Nimetembelea sehemu nyingi
duniani na kujifunza mengi.sasa ninatoa ujuzi huo kwa Wanafunzi wengine
ili nao waweze kupata nafasi kama mimi''.
Anaongeza;
''tofauti kubwa kati ya wasanii hapa na maeneo mengine duniani ni kuwa
hapa Watu wanafurahia wanachokifanya.Inawezekana tukawa hatuna ujuzi na
utaalam kama ilivyo kwa wasanii ya China na Urusi
HAMZA AKAMILISHA MATIBABU YAKE NCHINI MOROCCO
-
BEKI wa kati wa SimbaSC, Abdulrazack Mohamed Hamza amekamilisha matibabu ya
upasuaji ambayo yamefanyika nchini Morocco.
Hatua hiyo inampa Hamza matumaini...
Tuzo : Rais Mwinyi Apokea Tuzo
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein
Ali Mwinyi, ametoa wito kwa taasisi na wadau wa sekta ya utalii kuongeza
ushiri...
Post a Comment