|
Mwanasheria wa Vilabu Dr Damas Ndumbaru anasema Malinzi atasimamisha ligi kuu kwani vilabu havikubaliani na ubabe wake |
Muda
mfupi baada ya Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamali Emily
Malinzi kutangaza kuvibana vilabu vya ligi kuu kuchangia mapato yao kwa
asilimia tano ili kuchangia miradi mbalimbali iliyo anzishwa na
shirikisho la soka nchini, vilabu vya ligi kuu kupitia kwa mwanasheria
wao Dr Damas Ndumbaru vimetishia kugomea kuendelea na ligi kuu ya soka
inayoendelea hivi sasa na kumtaka Malinzi kuachana na agizo hilo ambalo
linaonekana lina lengo la kuvinyonya zaidi vilabu.
Akiongea
katika mazunguzo maalum na mtandao huu, Ndumbaru
amesema tayari amezungumza na wateja wake ambao ni vilabu na
wamekubaliana mambo kadhaa ikiwemo kuachana na ligi kuu pamoja na
kuelekea shirikisho la soka duniani FIFA endapo Rais Malinzi
atang'ang'nia msimamo huo.
No comments:
Post a Comment