Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, June 15, 2014

WORLD CUP 2014: IVORY COAST 2 v JAPAN 1, GERVINHO AWAPA USHINDI IVORY COAST

Japan ndio walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Ivory Coast usiku huu katika dakika ya 16 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Keisuke Honda.
Nao Ivory Coast walikuja kwa nguvu kipindi cha pili ndani ya dakika mbili waliweza kusawazisha na kufunga bao la ushindi.
W. Bony dakika ya 64 aliisawazishia bao Ivory Coast na muda mchache kupita baadae Y. Gervinho akawachinja Japan katika dakika ya 66' na kuwapa ushindi Ivory Coast.
Mechi inayofuata kwa Ivory Coast ni hapo Alhamisi na Colombia waliyoichapa Greece Bao 3-1 mapema Jana.
Japan watacheza na Greece Siku hiyo hiyo.
Gervinho na  Wilfried Bony waliipa ushindi  Ivory Coast  kipindi cha pili ndani ya muda mfupi wa dakika mbili tu na kuwasimamisha Wajapan.
Bony akiisawazishia bao  Ivory Coast
Nipe tano kwanza..... Bony akishangilia bao na  Didier Drogba pamoja na  Salomon Kalou baada ya kuwaunga na kuwa 1-1 wakitokea nyuma.
 Keisuke Honda ndie alikuwa amewamaliza kipindi cha kwanza dakika ya 16
Honda akiwatawanya mabeki na kipa na kuipa bao Japan
Honda akishangilia bao pamoja na wenzake
Yaya Toure akiwachomoka wachezaji wawili wa Japan
 Ivory Coast wakifanya yao
Salomon Kalou akipanga awatokeje wachezaji hawa wa Kijapan,  Shinji Okazaki akiwa amemkomalia...
Toure na Yuya Osako cwakikabana kwa karibu sana

VIKOSI:
Ivory Coast:
 Barry, Aurier, Bamba, Zokora, Boka (Djakpa 75), Tiote, Yaya Toure, Die (Drogba 62), Gervinho, Bony (Konan 77), Kalou.
Subs not used: Gbohouo, Viera, Kolo Toure, Bolly, Akpa Akpro, Diomande, Gradel, Sio, Sayouba.
Booked: Bamba, Zokora.
Goals: Bony 64, Gervinho 66.

Japan: Kawashima, Uchida, Morishige, Yoshida, Nagatomo, Yamaguchi, Hasebe (Endo 53), Okazaki, Honda, Kagawa (Kakitani 86), Osako (Okubo 68).
Subs not used: Nishikawa, Gotoku Sakai, Kiyotake, Aoyama, Konno, Inoha, Saito, Hiroki Sakai, Gonda.
Booked: Yoshida, Morishige.
Goals: Honda 16.
Attendance: 40,000
Referee: Enrique Osses (Chile)

No comments:

Post a Comment