
England imeshuka katika viwango vya ubora vinavyo tambuliwa na fifa mpaka nafasi ya 15 kwa mujibu wa viwango vipya vya ubora ikiwa ni nafasi ya chini kutokea tangu waliposhindwa kufuzu kwa michuano ya Ulaya ya mwaka 2008
Kushuka huko kwa nafasi sita kuna maanisha kuwa kikosi cha meneja Roy Hodgson sasa kimepitwa na Bosnia-Herzegovina, Ivory Coast na Greece katika msimamo wa ubora wa viwango vya soka duniani.Scotland imepanda kwa nafasi 24 mpaka kufikia nafasi ya 50 wakati ambapo Ireland ya Kaskazini imepanda kwa nafasi tano kutoka katika nafasi ya 111 ya mwezi JuniWales imeshuka kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 46 na Jamhuri ya Ireland ikishuka kwa nafasi tatu mpaka nafasi ya 44.

No comments:
Post a Comment