Rais wa TFF, Jamal Emil Malinz (kushoto) mkurugenzi wa Plan International, Jorgen Haldorsen (wa pili kushoto) wakitia sahihi katika mkataba huo mchana wa leo. (picha na Baraka Mpenja).
NDOA za utotoni zinawazuia mamilioni ya watoto wa kike nchini wasiweze kumaliza shule, kufikia ndoto zao katika maisha na kuwafanya waendelee kuteseka katika umasikini.
Kuna `mijibaba` inayoharibu watoto wa kike bila huruma na kama haitoshi inaamua kufunga ndoa za `kihuni` na watoto ambao ni taifa la kesho.
Serikali na mashiriki binafsi ya kutetea haki za watoto yanapambana dhidi ya tatizo hili, huku wazazi na watu wazima wakiwa sehemu ya tatizo.
Mpira wa miguu ni mchezo unaoongoza kuwa na mashabiki wengi nchini na dunia kote, hivyo mchezo huu unaweza kutumika kama njia ya kupambana na ndoa za utotoni.
Kwa kutambua mchango unaoweza kuletwa na mpira wa miguu, shirikisho la soka Tanzania, TFF limeingia ubia na shirika la kutetea haki za watoto la `Plan International` kwa ajili ya kutetea na kuhamasisha juu ya ulinzi wa haki za mtoto hapa nchini.
No comments:
Post a Comment