FA CUP: FULL TIME!!!! MANCHESTER CITY 1 v WIGAN 2, CITY HOI KWA WIGAN....!!! JORDI GOMEZ NA JAMES PERCH WAACHA KILIO ETIHAD USIKU HUU!!! WIGAN KUUMANA NA ARSENAL NUSU FAINALI MWEZI UJAO!
Dakika ya 53 City wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili, Yaya Touré anatoka na nafasi yake inachukuliwa na David Silva na Jesús Navas González nje nafasi yake inachukuliwa na Edin Dzeko ili waone kama watazirudisha bao hizo mbili katika kipindi cha dakika 30 zilizobaki! Nao Wigan wanafanya mabadiliko katika dakika ya 58 Callum McManaman anatoka nafasi yake inachukuliwa na James McClean.
Kipindi cha pili dakika ya 68 Samir Nasri akaipachikia bao City baada ya kuachia shuti kali na kufanya 2-1 Baada ya kupata krosi kutoka kwa Micah Richards. Mpira umemalizika Wigan wakiwa washindi kwa bao 2-1 dhidi ya City na ushindi huu unawakutanisha Wigan na Arsenal kwenye Nusu fainali ya FA CUP mwezi ujao wa Nne. Msimu uliopita, mara baada ya kutwaa FA CUP, Siku 3 baadae, Wigan waliporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu England na sasa wako Championship wakiselelea Nafasi ya 7 na wapo chini ya Meneja Uwe Rosler, aliekuwa Straika wa Man City kwenye miaka ya nyuma.
Aguero(katikati) akikabwa na wachezaji wawili wa Wigan'
Mchezaji Javi Garcia wa Man City akishikana shati na Callum McManaman wa Wigan kwenye kipindi cha dakika 45 za mwanzo..
Post a Comment