MANCHESTER UNITED WAFULIA UGENINI HAKUNA CHA RVP WALA ROONEY UGIRIKI,UEFA CHAMPIONS LEAGUE YAFUNGWA NA OLYMPIAKOS 2-0
Kipindi cha kwanza dakika ya 38 Manchester United wanafungwa bao na timu ya Olympiakos ya Ugiriki kwenye uwanja wao wa Karaiskakis Stadium, Jijini Athens, kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS. Mfungaji wa bao hilo akiwa ni Alejandro DomÃnguez baada ya kupata krosi kutoka kwa Giannis Maniatis na hatimae Alejandro kuugusa kwa kuuamisha uelekeo na kumfunga kipa wa United David De Gea na kufanya 1-0. Kipindi cha kwanza kinamalizika kwa bao hilo moja kutoka kwa Alejandro DomÃnguez.
Kipindi cha pili dakika 55 Mchezaji wa Olympiakos Joel Campbell akaiongezea bao la pili timu yake kwa kufanya 2-0 dhidi ya United baada ya mabeki wa United kufanya makosa ya ukabaji na hatimaye Joel Campbell kufunga bao hilo kwa kupewa pasi safi na Michael Olaitan.
Dominguez katikati akishangilia na bao lake la kwanza
Campbell akishangilia bao lake dakika chache baada ya kutoka mapumziko!
Baada ya kufungwa bao la pili United, Dakika ya 60 kipindi cha pili wamefanya mabadiliko Shinji Kagawa akaingia kuchukua nafasi ya Tom Cleverley na huku Danny Welbeck akichukua nafasi ya Antonio Valencia.
Post a Comment