Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 17, 2014

LA LIGA: GETAFE 0 v REAL MADRID 3, JESE, BENZEMA NA LUKA MODRIC WAJIWEKA VIZURI UGENINI

Real Madrid leo wameendeleza wimbi lao la kutofungwa na kufikia Mechi 25 na pia kuungana na Barcelona na Atlético Madrid kileleni mwa La Liga baada ya Jesé, Karim Benzema na Luka Modric kufunga Mabao wakiwa Ugenini walipocheza na Getafe.
Jana, Barca, ambao wanasaka Taji la Ubingwa la Tano katika Misimu 6, na Atletico Madrid zote zilishinda Mechi zao.
Barca wapo kileleni, wanafuatia Real na kisha Atletico, na hii ni kwa tofauti ya Magoli tu kwani wote wana Pointi 60 kila mmoja lakini, ikiwa watafungana mwishoni mwa Msimu, hiyo haimo na badala yake Bingwa atapatikana kwa kulinganisha Matokeo ya Uso kwa Uso kati yao.
Real, ambao hawajapoteza Mechi tangu wafungwe na Barca 2-1 huko Nou Camp Mwezi Oktoba, Leo walicheza bila ya Mfungaji wao Bora Cristiano Ronaldo, ambae yuko Kifungoni Mechi 3, walianza kufunga kwa Bao la Jese katika Dakika ya 6, kisha Dakika ya 27 Benzema akapiga Bao la Pili na Modric kupiga Bao la Tatu Dakika ya 66.
Hapo Jana, Barcelona waliifumua Rayo Vallecano Bao 6-0 na Atletico Madrid waliichapa Real Valladolid Bao 3-0.



MSIMAMO ULIVYO KWA SASA LA LIGA TIMU ZA JUU: 
2013/2014 Spanish Primera División Table

Overall
Home
Away

POS
TEAMPWDLFA
WDLFA
WDLFA
GDPts
1 Barcelona 24 19 3 2 69 17
11 0 1 42 9
8 3 1 27 8
52 60
2 Real Madrid 24 19 3 2 68 24
10 0 1 36 10
9 3 1 32 14
44 60
3 Atletico Madrid 24 19 3 2 59 16
11 2 0 41 7
8 1 2 18 9
43 60
 
RATIBA/MATOKEO
Ijumaa Februari 14

Elche CF 0 v Osasuna 0
Jumamosi Februari 15
Atletico de Madrid 3 v Real Valladolid 0
Levante 1 v UD Almeria 0
FC Barcelona 6 v Rayo Vallecano 0
Villarreal CF 0 v Celta de Vigo 2
Jumapili Februari 16

Granada CF 1 v Real Betis 0
Getafe CF 0 v Real Madrid 3

Athletic de Bilbao 1 v RCD Espanyol 2
23:00 Sevilla FC v Valencia
Jumatatu Februari 17
24:00 Malaga CF v Real Sociedad

No comments:

Post a Comment