TIMU ya
African Lyon imejiweka katika nafasi nzuri ya kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara
baada ya kuifunga timu ya Villa Squad bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi daraja la
kwanza uliochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani juzi.
Mchezo huo
wa raundi ya pili ulikuwa wa ushindani kwani kila timu ilijitahidi kupambana
walau iondoke na pointi tatu lakini hadi mapumziko hakuna timu iliyokuwa
imeliona lango la mwenzake.
Kipindi cha
pili kila timu ilifanya mabadiliko lakini African Lyon ndio ilifaidika na
mabadiliko hayo kwani dakika 70 ilipata
bao lililofungwa na Mike Mbela
Akizungumza
kwa simu kocha wa African Lyon Charles Otieno alisema kuwa anashukuru ameshinda
mchezo huo kwani ulikuwa na ushindani na rafu za hapa na pale.
“Mchezo wetu
na Villa ulikuwa mchezo mgumu lakini nashukuru wachezaji waliweza kufanya kile
nilichowaelekeza kufanya na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu”, alisema Otieno
Kwa matokeo
hayo African Lyon imefikisha pointi 17
na mchezo ujao itacheza na Tesema kwenye Uwanja wa Karume, Ilala.
No comments:
Post a Comment