Ross
Barkley, amefunga Bao katika Dakika ya 84 kwa Frikiki murua nakuipa
ushindi Everton walipoichapa Swansea City, waliokuwa kwao Liberty
Stadium, Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Bao
la kwanza la Mechi hii lilifungwa kwa kiki kali ya Fulbeki wa Everton,
Coleman, katika Dakika ya 66 lakini lilidumu kwa Dakika 4 tu kwani
Fulbeki wa Swansea, Tiendalli, alipanda juu na jaribio lake lililokuwa
linaenda nje kumbabatiza Oviedo na kutinga na kuifanya Gemu iwe 1-1.
Ndipo
ikaja Frikiki ya Ross Barkley iliyowapa ushindi Everton na kuwafanya
wawe hawajapoteza Mechi yeyote katika Mechi 10 na kupanda hadi Nafasi ya
4 kwenye Msimamo wa Ligi. 
Steven Pienaar na Ben Davies wakichuana vilivyo leo kwenye ligi kuu England

Majanga: Jose Canas na Gareth Barry

Wilfried Bony na Barkley wakionesha ubabe nani akatize nani apoteze mpira

Wakipoteza nafasi ya kufunga bao...na hapa mchezaji anajiuliza zaidi kupoteza nafasi hiyo iliyokuwa wazi

Baadae Everton wakazinduka na mchezaji Seamus Coleman akaipatia bao

Raha ya ushindi kupongezwa!!! baada ya kupata bao hapa


Swansea wakisawazisha bao na hapa anashangilia bao

2-1 mpaka ndani ya nyavu..
Post a Comment