MWANANYAMALA MABINGWA WA KOMBE LA MEYA WA KINONDONI, WAKABIDHIWA BAJAJI, FEDHA TASLIMU MILIONI 2 NA JEZI
Na Fadhili Akida
Mwananyamala mabingwa wa kombe la meya wa kionondoni dhidi ya kawe kombaini, wakabidhiwa bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi katika fainali iliyofanyika uwanja wa magunia, msasani dar es salaam.
Timu ya soka ya Mwananyamala jana waliibuka mabingwa wa kombe la meya wa kinondoni na kukabidhiwa zawadi za bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi. akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, januari makamba aliwaasa vijana hao kutumia vema zawadi hizo ikiwemo fedha na bajaj kwa kusaidia maendeleo yao ikiwemo kuboresha maisha yao. makamba alimsifu meya wa manispaa hiyo yusuph mwenda kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yanasaidia kuwaleta vijana pamoja na kudumisha mshikamano na amani baina yao. kwa upande wake meya wa manispaa hiyo, yusuf mwenda alisema huo ni mwanzo tu wa kampeni yake ya kuweka safi manispaa yake ambapo kupitia michezo anawahamasisha wakazi wa manispaa hiyo kuweka safi mazingira yanayowazunguka.
Post a Comment