Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, October 7, 2013

KINDA LA UNITED ADNAN JANUZAJ SASA NI "DILI" ROY HODGSON ATAKA ACHEZEE TIMU YA TAIFA.


KINDA wa Manchester United Adnan Januzaj, ambae Jumamosi aliipa ushindi Klabu yake katika Mechi yake ya kwanza kabisa kuanza alipopachika Bao zote mbili walipoifunga Sunderland 2-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, sasa anafuatiliwa na England kwa mujibu wa Kocha wa Nchi hiyo Roy Hodgson.
Hodgson amesema: “Ukweli ni kwamba ni Kipaji cha kweli na tunamtazama lakini mambo mengi yanabidi yajadiliwe. Yupo na Man United kwa muda mrefu na inabidi kujadiliana kwa muda mrefu.”
Januzaj, mwenye Miaka 18, ambae Asili ya Wazazi wake ni Kosovo lakini Raia wa Albania, kwa sasa anaweza kuzichezea Nchi kadhaa zikiwemo Belgium, Albania na Turkey.
Ili kuichezea England inabidi apate Uraia wa Kujiandikisha au kuhalalishwa baada ya kuishi muda mrefu England.


Januzaj akipongezwa baada ya kufunga bao mbili peke yake na kuibeba United Juzi na hapa alikuwa akipongezwa na Robin van Persie na Michael Carrick
Bosi wa Manchester United David Moyes amekiri kuwa FA ya England imewasiliana na Old Trafford kuhusu Januzaj kuichezea England.
Moyes amekiri: “Ndio. Ipo njia ya yeye kuichezea England kupitia yeye kuishi muda mrefu hapa.”
Januzaj ameitwa mara kadhaa kuichezea Belgium lakini amekuwa akikataa huku duru za ndani zikidai mapenzi yake ni kuichezea Nchi ya Asili ya Wazazi wake Albania.
Kipa wa Sunderland akifungwa na Januzaj juzi jumamosi.Roy Hodgson akiwa anateta na viongozi wa soka kuhusu kumsogeza huyo Kinda England ili achezee timu ya Taifa ya Nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment