FULHAM ILIPOIFUMUA CRYSTAL PALACE 4-1 KATIKA MCHEZO WA ENGLISH PREMIER LEAGUE NYUMBANI KWAO
Mchezaji wa Crystal Palace Mariappa ndio ameanza kuifungia timu yake dakika ya 7 kabla ya Kasami wa Fulham kusawazisha bao hilo katika dakika ya 19.
Dakika za mwisho kipindi cha kwanza dakika ya 45 Fulham walipiga frii kiki na ukuta wa Crystal Palace wakazuia na mchezaji wa Fulham Sidwel akamalizia mpira huo kwa shuti kali mpaka langoni mwa lango la Crystal na kipa wao kutoona ndani na mpira kumalizika kipindi cha kwanza Fulham wakiongoza kwa 2-1dhidi ya wenyeji.
Kipindi cha pili dakika ya 50 Krosi safi kama kona na Dimitar Babatov akaunganishia nyavuni kwa ndoo na kuandika bao la tatu.
Kipindi cha pili hicho hicho dakika 55 Mchezaji Senderos aliyeingia kipindi cha pili akatupia tena bao la nne huku kipa akiuokolea ndani ya lango lake.
Post a Comment