LONDON, England
KLABU ya Liverpool bado imeweka ngumu kumwachia nyota
wake, Luis Suarez ang’oke kwenye klabu hiyo.
Wakati
Liverpool ikiweka ngumu, nyota wengine Ulaya mambo yameshawanyookea, baada ya
kusaini mikataba mipya ama kuhamia kwenye klabu nyingine.
Miongoni
mwa wachezaji ambao mambo yao yameshakuwa safi ni pamoja na mfungaji bora wa
ligi ya Bundesliga msimu uliopita,
Stefan Kiessling, ambaye amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Bayer
Leverkusen, huku Robert Lewandowski akijiandaa kujiunga na Bayern Munich msimu
ujao, wakati Stevan Jovetic, Gonzalo
Higuain, David Villa na Alvaro Negredo wote wakiwa wameshakamilisha usajili.
Mbali
na wachezaji hao, timu ya Juventus yenyewe imeshamnasa Fernando Llorente na
nyota wa Manchester City, Carlos Tevez,
ambao ni kati ya nyota wazuri Ulaya.
Hata
hivyo, endapo kocha Brendan Rodgers ataamua
kumuachia aondoke kwenye klabu hiyo ya Anfield, swali lililopo ni kwamba
ni nyota gani atakuwa mbadala kwa Suarez?
Kwa
mujibu wa wachambuzi wa masuala ya soka, wanaangazia wachezaji saba ambao
wanaweza kuziba pengo la Suarez endapo ataondoka.
Jackson Martinez
Mcolombia
huyo mwenye misuli, Martinez msimu
uliopita alifunga mabao 26 katika
mechi 30 alizoichezea FC Porto na mabao
hayo ndiyo yalimfanya kuwa mchezaji anayewindwa kwa udi na uvumba katika soko
la usajili.
Inaelezwa
kuwa endapo Suarez ataondoka, inambidi Rodgers
kwa haraka kukimbilia kumsajili nyota huyo hususan baada ya Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis naye kuthibitisha nia
ya kumsajili.
Inaelezwa
pia uwezo wa kutoa pasi na nguvu alizonazo unaweza kuwa msaada mkubwa kwenye
kikosi cha Liverpool.
Luis Muriel
Akiwa
tayari ameshaonesha uwezo kama mchezaji raia mwenzake, Falcao na nyota wa
Brazil, Ronaldo, Muriel anatajwa
kuwa hazina kwenye mechi.
Mwaka
jana katika msimu wake wa kwanza akiwa na timu ya Udinese aliweza kupachika
mabao 11 na mara kadhaa amekuwa akitolewa macho na klabu kubwa.
Inaelezwa
kuwa akiwa na umri wa miaka 22, huenda akawa hazina kwa timu hiyo endapo kocha
wake ataamua kumnunua.
Roberto Soldado
SOLDADO ameshadhihirisha uwezo wake wa kuweka rekodi,
baada ya kufunga mabao 81 katika
mechi 141 alizoichezea Valencia.
Tayari
kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas ameshakiri kummezea mate mshambuliaji
huyo, lakini klabu hiyo ya Hispania imeshaweka ngumu hadi dau lake la pauni
milioni 26 litakapokamilika kabla ya kumuachia aondoke.
Inaelezwa
kuwa kuwa hata kama hataweza kuwa mbadala halisi wa Suarez, lakini kwa uwezo wa Mhispania huyo
aliouonesha hivi karibuni unakuwa na uhakika wa hela yako kurudi.
Oscar Cardozo
Kinara
huyo raia wa Paraguay aliwateka
mashabiki wa Benfica baada ya kupachika
mabao misimu yote sita mfululizo aliyoichezea timu hiyo ya Estadio da Luz.
Hata
mwishoni mwa msimu uliopita alijikuta kwenye wakati mgumu, baada ya kukwaruzana
na kocha wake, Jorge Jesus.
Kutokana
na uwezo wake, Fenerbahce inatamani kumsajili Cardozo ambaye pia anawindwa na
timu ya Cardiff City, lakini ikakataa
kutoa ofa zaidi ya milioni 13 kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
Inaelezwa
kuwa mwajiri wake huyo Mreno anasemekana anataka kitita cha pauni milioni 15
ili imwachie nyota huyo ambaye licha ya kutokuwa na uwezo mkubwa wa kutoa pasi,
lakini anaweza kufanya makubwa kwenye kikosi hicho cha Anfield.
Leandro Damiao
Mshambuliaji
huyo wa timu ya Inter Milan, Mbrazili mwenye umri wa miaka 24, ameshindwa
kuonesha cheche zake kwenye kikosi cha timu ya taifa kama alivyo shujaa Fred kutokana na kukumbwa na majeraha ya mara
kwa mara.
Akiwa
anawindwa kwa muda mrefu Spurs, Damiao
wakati mwingine amekuwa akiwindwa na vigogo kadhaa vya Ligi Kuu, lakini klabu yake imekuwa
ikiweka ngumu kumuuza kwa bei chee.
Inaelezwa
kuwa licha ya kukumbwa na majeraha, lakini endapo atatumika vilivyo anaweza
kuwa tishio kwa mabeki.
Pablo Osvaldo
Mshambuliaji
huyo, Osvaldo amekuwa akihusishwa kuhamia katika timu za Fulham na Valencia, lakini hakuna makubaliano
yaliyofikiwa.
Akiwa
na umri wa miaka 27, msimu uliopita
aliifungia timu yake ya AS Roma mabao 16
kwenye michuano ya Ligi ya Serie A na ameshaichezea mara nane timu ya
Taifa ya Italia.
Inaelezwa
kuwa endapo Rodgers atamnyakua mzaliwa huyo wa Argentina, anaweza kuwa msaada
mkubwa kwake kama ilivyo kwa Suarez.
Fred
Akiwa
na umri wa miaka 29, anaweza kuwekwa
kando kwa wachezaji chipukizi wa Rodgers.
Lakini
hata hivyo inaelezwa mshambuliaji huyo bado ana uwezo wa kufanya makubwa.
No comments:
Post a Comment