MSHAMBULIAJi mpya wa Manchester United, Wilfried Zaha alikuwa kituko wakati timu hiyo inaondoka Uwanja wa Ndege kwa ziara yake ya Mashariki mbali kujiandaa na msimu mpya.
Wakati wachezaji wenzake wote walifika Uwanja wa Ndege wakiwa wamevaa suti za klabu na tai, Zaha, ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Crystal Palace, lazima atakuwa hakupata ujumbe kuhusu vazi.
Kivyake: Mchezaji mpya wa Manchester United, Wilfried Zaha alikuwa mchezaji pekee aliyewasili amevaa kivyake
Vazi la disko: Zaha alipiga T-shirt, jinzi na raba
Winga huyo wa England aliteremka katika gari lake akiwa amevaa fulana nyeupe na jinzi na raba, akisema amepoteza nguo zake za zamani.
Alilazimika kuomba walinzi wa United kumpatia suti nyingine na kisha akabadilisha pale pale Uwanja wa ndege kabla ya kukwea pipa.
Zaha ni sehemu ya msafara wa watu 198, wakiwemo makocha, wachezaji na viongozi waliosafiri kwenda Bangkok kwa ajili ya mechi ya kwanza kati ya tano za ziara ya Asia na Australia.
Alibadili haraka: Zaha alionekana vizuri na mwenye furaha baada ya kuvaa suti
Wachezaji waliwasili saa 1:00 usiku ikiwa ni saa mbili kabla ya ndege kuondoka.
Miongoni mwa wachezaji walioondoka ni Wayne Rooney, ambaye amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kuondoka Old Trafford majira haya ya joto, kuhamia kwa wapinzani wa Ligi Kuu England, Chelsea.
Kwa sasa anabakiwa kuwa mchezaji wa United na anatarajiwa kuwamo katika kikosi kitakachocheza mechi ya kwanza dhidi ya Singha All Star XI mjini Bangkok Jumamosi.
Kocha David Moyes amesema katika mahojiano na Radio mapema Jumatano ya leo kwamba alikuwa ana vikao vinne na mchezaji na amemuahidi atabaki.
Kwenye ndege: Wayne Rooney (kushoto) na Moyes kulia safarini leo
Makocha: Ryan Giggs na Phil Neville kulia
Watanashati: Rio Ferdinand (kushoto) na Patrice Evra kulia
Wako poa: Kutoka kushoto, Fabio da Silva, Alexander Buttner, Danny Welbeck, Phil Jones na Rafael da Silva
Daraja la kwanza: Kutoka kushoto, Fabio da Silva, Buttner, Welbeck na Jones
No comments:
Post a Comment