MADRID,
Hispania
WAKATI mchakato
wa usajili ukizidi kupamba moto Ulaya, baadhi ya
Ligi zimeonekana kulitilia maanani sakata hili. Ligi Kuu Hispania, ni moja ya
Ligi zilionesha nia ya kuvalia njuga usajili, huku kukiwa na idadi kubwa ya
nyota kusaini na wengine kuondoka.
Tayari timu
zimemwaga mamilioni kuvinoa vikosi vyao kabla ya kuanza kwa msimu mpya, ingawa
muda unaruhusu kuleta vifaa na kutoa mizigo.
Makala haya yameangazia, nyota
nane ambao mpaka sasa wametishia katika uhamisho huu. Wakiajiliwa na wengine
kuondoka.
Radamel
Garcia Falcao
Anabaki kuwa
mchezaji aliyesajiliwa kwa kikita kikubwa msimu huu, baada ya kusaini Monaco ya
Ufaransa akitokea Atletico Madrid ya Hispania kwa ada ya euro mil.60.
Falcao
"El Tigre" alikuwa akiwindwa na vigogo kadhaa Ulaya, lakini aliacha
gumzo baada ya kukubali ofa ya timu iliyopanda daraja msimu huu.
Alikuwa
na kila kigezo cha kuchezea timu yoyote ile hapa duniani, kutokana na kiwango
alichoonesha tangu atue Atletico Madrid, huku akifunga mabao 52 katika michezo 67 msimu uliopita.
Neymar
da Silva Junior
Wakati kinda
huyp wa Brazili aliposaini Barcelona, mwanzoni mwa mwezi Juni, mabeki wa timu pinzani, hazitia wasiwasi ujio wake.
Neymar
alijiunga na Barca kwa ada ya euro mil.57 akitokea Santos ya Brazil, lakini
alianza kuzitia hofu timu pinzania baada ya kuonesha maajabu kwenye michuano ya
Kombe la mabara lililofanyika Brazil. Aliongoza nchi yake kutwaa kombe huku
yeye akiibuka mchezaji bora wa michuano. Amekwenda Camp Nou anakutana na mchawi
wa soka duniani, Lionel Messi, lazima wakae.
“Ilikuwa ndoto yangu muda mrefu kutua Nou Camp. Na leo ndoto imetimia.
Sikuwahi kufikiria kuja hapa kwa nia ya kuwa mchezaji bora, kama ni mchezaji
bora yuko hapa- Messi” alisema Neymar wakati akitambulishwa Camp Nou.
Isco
Francisco
Roman Suarez ‘Isco’, amejiunga na Real Madrid kwa kiasi cha euro mil.30 akitokea
Malaga ya nchini humo pia.
Ni
miongoni mwa Yosso walio kwenye kiwango cha juu kwa sasa nchini Hispania, na
hii ni kutokana na mafanikio yake ya kuifuikisha Malaga robo fainali kwenye
michuano ya Uefa, ikiwa ni ni mara ya kwanza kwa timu hiyo.
Lakini
amezua utata, baada ya kumdharirisha Lionel Messi kwa kumfananisha na mbwa.
“Nilimwita
mbwa wangu jina la Messi, sababu Messi ni mchezaji bora wa dunia,hivyo Messi ni mbwa wangu”, lilipoti gazeti
la Metro.
Jesus
Navas
Winga huyo ametua Manchester City ya
England akitokea klabu ya Sevilla kwa ada ya uhamisho wa euro mil.17.5 Juni.
Uhamisho
wake ulikuwa gumzo kote, kutokana na imani ya wachezaji wa Kihispania kupenda
kucheza nyumbani.
City, hupendelea
soka la kizamani kumuona mchezaji anakaba na kufunga mara zote, ila Navas sio
mtu wa namna hiyo, kwani alishindwa kuthibitisha hilo akiwa Sevilla.
Benat
Etxebarria
Benat ameamua
kuirudia timu yake ya zamani Athletic Bilbao, baada ya kukubaliana na Real
Betis kwenda kwa euro mil.8.
Mkataba
wa miaka mitano aliyposainisha umezivunja moya timu za West Ham na Bolton za
England zilizokuwa zikinyemelea saini yake.
Kiungo huyo
‘aliweka ngumu’ kusaini tena Betis, hali iliyowafanya kumuuza kuliko kuondoka
kama mchezaji huru msimu ujao.
Dani
Carvajal
Amejikuta akirejea nyumbani Santiago Bernabeu, baada ya kuishi Ujerumani
kwa miaka kadhaa akiwa Bayern Leverkusen. Ni zao la akademi ya Madrid, kabla ya
kujisafishia nyota na kuitwa timu ya kwanza muda mfupi.
Msimu mmoja
baadae. Madrid walimuuza kwa euro mil.5, lakini wamelazimika kumrejesha kwa
euro mil.6.5 kutokana na kiwango chake kupanda kwa kasi.
Leo
Baptistao
Atletico
Madrid wanasubiria ahadi aliyotoa nyota
huyo raia wa Brazil. Safari yake kutoka Rayo Vallecano kwenda Atletico,
hata kwa mguu angetembea. Ni majirani sana.
Amesainishwa
kwa uhamisho wa euro mil.7, baada ya kuichezea Vallecano mechi 28 tu msimu
uliopita.
“Nina furaha kubwa kurejea kwetu.
Naahidi kujitolewa kwa lolote Atletico na kujifunza mengi . Bado mie ni kijana
mdogo, miaka 20,”
David Villa
Anaungana na Baptistao Atletico
Madrid katika mbio za kuwinda ubingwa wa
La Liga. Villa anakuwa mbadala wa Falcao aliyetimkia Monaco kwa ada ya uhamisho
wa euro mil.5 akitokea Barcelona.
Nyota huyo (31), alisaini Barca 2011, akitokea Valencia, lakini
ameshindwa kwendana na kasi ya Wana-Catalunya hivyo kupigwa benchi mechi
nyingi.
Bado vuguvugu linaendelea, huenda mastaa kuongezeka ama kupungua La Liga
No comments:
Post a Comment