RIO DE JENEIRO, Brazil
MSHAMBULIAJI wa timu ya
Taifa ya Brazil na Santos, Neymer ni kati ya wachezaji ambao usajili wake msimu
huu umetikisa kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Usajili huo ulivitikisa
vichwa vya mashabiki mbalimbali wa soka kutokana na nyota huyo kuwindwa na timu mbalimbali
kubwa barani Ulaya.
Hata hivyo kitendo
cha nyota, kujiunga na Barcelona ya
Hispania, kimezua sintofahamu katika klabu ya Santos alikotokea.
Moja ya wahisani wa
Neymar, Kampuni ya Supermarket 'DIS'
nchini humo inaamini nyota huyo alistahili kuuzwa kitita kikubwa cha fedha
zaidi ya euro milioni 57 walizoopewa.
Licha ya uhamisho huo, DIS
inayomiliki asilimia 40 kwa kinda huyo,imesema haijapewa 'kilicho chao' katika
uhamisho wa kinda huyo na kutishia kuchukua hatua za kisheria ili kupata haki
yao.
Kiongozi wa kampuni hiyo,
Idi Sonda, hivi karibuni aliilalamikia Santos kukubali ofa hiyo, wakati awali
walikubaliana Barca kuongeza dau.
Hata hivyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa DIS Roberto Moreno, amewataka kuufunga mjadala kuhusu uhamisho wa
Neymar (21) na kuahidi kuchukua hatua za kisheria itakapobidi.
Kasheshe hiyo, imechochewa
na tetesi zilizozagaa, kwamba Santos italipwa kiasi cha euro mil.2, endapo
mchezaji huyo ataingia kwenye orodha ya wachezaji watatu watakao wania tuzo ya
mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or msimu huu.
Santos, itaingiza
kibindoni mapato yatakayopatikana kwenye mchezo wa kirafiki uliopagwa na timu
zote , huku Barca wakilazimika kulipa euro mil. 4.5 endapo mechi hiyo
haitafanyika.
Inaonekana Santos wanataka
kupiga dili hilo kimya kimya, ikiwa mpaka sasa DIS hawajapewa taarifa hizo.
Hali ilizua vurumai baina ya wawili hao.
Moreno, amebainisha
mpaka sasa DIS, haikupokea hati (dokumenti) yoyote ya uhamisho wa Neymar.
“Sijawahi kuoneshwa hati
hata moja, nataka niwafuate Santos, halafu ndipo nitaamua kama tutakwenda
mahakamani ama la!,” Moreno alisema.
Tovuti moja nchini humo,
juzi ilitoa taarifa kampuni hiyo kuwa kwenye mipango ya kulifikisha suala hilo
mahakamani.
Mwezi uliopita, Moreno
aliwatishia klabu zote Santos na Barcelona, na kutoa onyo kali kwa kuwapa wiki
moja kabla ya kufungua shitaka kutaka kujua mpango walionao Santos".
DIS, waligharimikia euro
mil 2.6 katika usajili wake 2009, ambapo kujiunga kwake na mabingwa wa Hispania,
wangeingiza euro mil.6.8 kutokana na asilimia 40 wanazo miliki.
Santos, ilipata faida ya
euro mil.17 huku euro mil.40 zilikwenda sehemu nyingine ikiwemo familia ya
mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment