Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 11, 2013

UGANDA CRANES KUTUA DAR LEO


Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili nchini  leo tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

The Cranes itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda ambapo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Burundi nao watawasili kesho saa 9.35 kwa ndege ya Kenya Airways. Naye Kamishna wa mechi hiyo Tesfaye Gebreyesus kutoka Eritrea atatua nchini keshokutwa alfajiri kwa ndege ya EgyptAir.

Maofisa wote hao wa mechi hiyo watafikia hoteli ya New Africa. Mkutano wa maandalizi ya mechi utafanyika Ijumaa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa, na utakuwa chini ya Gebreyesus.

No comments:

Post a Comment