Swansea City wanatarajiwa kumsajili mshambuliaji mduchi Wilfried Bony kutoka Vitesse Arnhem zoezi ambalo huenda likamalizwa hii leo.
Mpango huo huenda ukagharimu kiasi cha pauni milioni £13 kutegemeana na mahitaji mengine binasfi yaani maslahi binafsi ya mchezaji huyo aliyefunga jumla ya mabao 31 katika jumla ya michezo 30 aliyocheza msimu uliopita.
Hawa ni wale waliosajiliwa kiangazi na meneja wa Swansea City Michael Laudrup
Jonjo Shelvey akitokea Liverpool (£5m)
Alejandro Pozuelo akitokea Real Betis (undisclosed fee)
Jose Canas akitokea Real Betis (free)
Jordi Amat akitokea Espanyol (£2.5m)
Jonathan de Guzman akitokea Villarreal (season-long loan)
Gregor Zabret akitokea NK Domzale (undisclosed fee)
Alex Gogic akitokea Olympiakos (free)
West Ham pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ivory Coast lakini Swansea wakionekana kuwa vinara wa mbio hizo.
Uwekezaji huo katika kikosi umeonekana kuchagizwa zaidi na meneja Michael Laudrup, ambaye amesema Liberty Stadium itabidi kuimarika katika msimu wa 2013-14 katika muendelezo wa mafanikio ya msimu uliopita.
Swansea ilishinda kikombe cha Capital One kwa kuzifunga Liverpool na Chelsea katika safari ya kuelekea kutwaa taji hilo ambapo wameingia katika michuano ya Europa League huku wakimaliza katika nafasi ya risa katika ligi kuu ya England Premier League.
No comments:
Post a Comment